.

.

.

.

Saturday, November 22, 2008

WAZEE WANYIMWA VISA KUINGIA ZIMBABWE

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan na aliyekuwa Rais wa Marekani Jimmy Carter wameahirisha safari waliokusudia ya kwenda nchini Zimbabwe.
Viongozi hao wamesema serikali ya Zimbabwe imewanyima viza ya kuingia nchini humo.
Kukosa viza hizo kumesababisha safari yao ya siku mbili pamoja na ya mke wa Bw Nelson Mandela, Graca Machel kushindikana.
Viongozi hao watatu wa kimataifa ni sehemu ya kundi linaloitwa 'Elders' lililoundwa ili kutatua migogoro ya dunia.
Hapo awali, serikali ya Zimbambwe ilikana ripoti iliyosema kuwa nchi hiyo ilikuwa ikifanya jitihada ya kuzuia ziara hiyo.
Bw Annan aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Johannesburg, " Ilibidi tuahirishe ziara yetu kwasababu serikali ya nchi hiyo imeweka wazi kuwa haitoshirikiana nasi."

No comments:

Post a Comment