.

.

.

.

Friday, October 31, 2008

THE QUEENS AT STEAM BAR


KIMWANA WA WIKI


VOODOO THREATS ON LEWIS HAMILTON

Championship leader Lewis Hamilton has again been targeted by Spanish racists in the build-up to this weekend's title-deciding Brazilian Grand Prix.
World governing body the FIA and Hamilton's McLaren team have condemned a 'voodoo-style' website aimed at wrecking Hamilton's championship dreams.
The 23-year-old goes into Sunday's showdown at Interlagos needing only to finish in the top five to become the youngest champion in Formula One history.
But ahead of the race, racism is again threatening to overshadow the event as hundreds of abusive messages have been posted on a website in Spain.
The website carries the name Pincha la Rueda de Hamilton, which translates as Burst Hamilton's Tyre.
Visitors to the site, with 20,000 to date, are encouraged to drop imaginary nails, pins or porcupines on a mock-up of the Interlagos circuit.
A notice on the site reads: "Hamilton can't finish the race. We have to stop him however we can.
"All you have to do is choose a spike, place it where you want on the circuit and hope he suffers a historic puncture."
On leaving the website, an automated message informs visitors: "We hope Hamilton punctures thanks to your help."

EPA IMEKUWA HAIEPEKI


Ukisikia namna ile mijamaa iliyojichotea mabilioni ya pesa kutoka Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA ilivyohaha jana kurejesha pesa hizo kabla ya kipenga kupulizwa leo, walahi utadhani ni simulizi za kubuni za elfu lela ulela! Ilikuwa patashika nguo kuchanika kwenye mabenki. Kwa mahesabu ya haraka haraka, inadaiwa kwa jana tu, shilingi 17,000,000 zililerejeshwa. Habari za kuaminika zinadai kuwa, mapesa hayo yalibwagwa benki jana alasiri na kutokana wingi wake, makarani wakayahesabu hadi usiku wa manane. Kwa mujibu wa taarifa toka kwenye tawi la benki moja maarufu Jijini (jina linalihifadhiwa), mapesa hayo yaliyokuwa kwenye maboksi ya mbao, mengi yakiwa ya noti za alfu kumi-kumi na alfu tano. ``Haikuwa kazi rahisi. Noti zenyewe zilikuwa ni nyingi mno na zilifikishwa katika muda ambao tayari wengine walishachoshwa na shughuli za mchana... wakajikuta wakikesha kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo ambalo lilianza muda mbaya wakati benki zinakaribia kufungwa,`` kikadai chanzo chetu. Imedaiwa kuwa mmoja wa wahusika hao alirejesha kiasi cha shilingi bilioni 12 taslimu na mwingine akarejesha bilioni tano. Watu hao ni miongoni mwa waliokuwa wakitajwa tajwa kujichotea mapesa hayo. Imedaiwa kuwa pesa hizo zilifikishwa katika tawi la benki hiyo zikiwa katika magari mawili ambayo yalifika kwa nyakati tofauti na kupakua maboksi yaliyosheheni minoti hiyo. Urejeshwaji huo wa staili ya aina yake, ulifanyika zikiwa zimesalia saa chache kabla ya kufika tarehe ya mwisho aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete kwa waliochota pesa hizo kuwa wamezirejesha.

RAY C KUFUNGA PINGU ZA MAISHA ?

Mwanadada nguli katika uimbaji na kunyonga kiuno chake nchini Tanzania Rehema Chalamila AKA Ray C . anatazamiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake Lord Eyez wa kundi la Nako2Nako .Wakizungumza kwa kupokezana, wapendanao hao walidai wanaamini kuwa muda umefika wa kufunga pingu za maisha na kuishi kama mke na mume.“Tunamalizia kurekodi nyimbo zetu. Albamu yangu inaitwa ‘Coming of the Real King’ na ya Ray C inaitwa ‘Touch me’. Tukimaliza kurekodi kitakachofuata ni kufunga ndoa tu,” alieleza Lord Eyez.Kauli hiyo ya kuiva kwa mikakati ya kufunga ndoa ilionekana kumfurahisha zaidi Ray C ambaye alikuwa ubavuni mwa Lord Eyez huku akitabasamu na kuchombeza maongezi hayo.“Ni kweli tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Muda utakapokaribia tutakuita ili uje kuchukua picha nzuri zaidi za ndoa yetu,” alisema Ray C kwa furaha.Wapenzi hao walibambwa wakipeana maraha ‘chobingo’ usiku wa manane ndani ya Viwanja vya Leaders Club, ambapo siku hiyo kulikuwa na tamasha kubwa la Inter College Bash.

JOTO LA MBAGALA


Wakazi wa Mbagala kufa hawafi lakini cha moto wanakipata . Kwa muda sasa maji yanakuwa na mgogoro kutokana na ujenzi wa barabara ya Kilwa ambao umetafuna mabomba yaliyopo. Naam wataalamu walitakiwa kujua kwamba mabomba hayo yanazikwa pande hii na pande ile yakiwa na umbali wa kutosha kutoka barabarani. Lakini wataalamu wetu hawakufanya hivyo, wao walikuwa wanaona miaka miwili tu hawajui kwamba ipo siku kitu fulani kitahitajika. Tutajifunza lini mipango miji. Picha kwa hisani ya lukwangule

UKWELI AU USANII WA SELIKALI KUJULIKANA LEO


Mwanasiasa mkongwe nchini na Naibu Gavana wa zamani wa BoT, Bob Nyanga Makani, amesema kuwa leo ndio ukweli au usanii wa serikali utajulikana. Makani, ambaye pia aliwahi kuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali katika awamu ya kwanza, alisema alishangaa, anashangaa na atashangaa zaidi iwapo tuhuma hizo za wizi wa fedha za EPA zitazidi kufanywa kuwa madai badala ya jinai.
Makani, ambaye ni mtu aliyewahi pia kushika nyadhifa mbalimbali za ujumbe na uenyekiti wa bodi mbalimbali za mashirika na taasisi za umma, alisema kilichofanyika BoT ni jinai na kwamba matumaini ya Watanzania ni kuona watu wanakamatwa.
"Si tuhuma za madai zile, ni makosa ya jinai, watu wameiba fedha huwezi kuwafanyia kesi ya madai," alisema Makani na kuongeza:
"Lakini siku si zimekwisha! Kuna kitu gani... hebu tumsubiri Kikwete tuone atafanya nini kama alivyosema mwenyewe, tusimhukumu kabla."
Duru za kiserikali zinasema baadhi ya akaunti za vigogo wa makampuni yaliyochota mabilioni hayo kwa mgongo wa wafanyakazi wadogo, zimeweza kuchunguzwa na fedha kuchukuliwa.
Taarifa hizo zinasema kukamatwa kwa akaunti za vigogo hao kunatokana na kuangalia mzunguuko mzima wa fedha kutoka malipo yaliyofanywa BoT hadi zilizoishia.
"Hawa watu walitumia wafanyakazi wao kusaini fedha, lakini uchunguzi uliona mwisho wa fedha ziliingia katika mikono ya vigogo kwa kuingia katika akaunti zao," kilidokeza chanzo huru kutoka duru za kiserikali."
Kwa mujibu wa duru hizo, iwapo rais ataamua kutumia mamlaka yake kufikisha wote waliohusika mahakamani, basi kuna vigogo ambao ni wafanyabiashara wakubwa, mawakili maarufu na baadhi ya maafisa wa serikali, watakumbwa na zahama hiyo.
Ufisadi wa EPA ulibainika katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, baada ya ukaguzi uliofanywa na kampuni ya Ernst& Young, ambayo ilipewa kazi iliyoachwa kiporo na Deloitte&Touche ya Afrika Kusini iliyositishwa ghafla kuendelea na ukaguzi huo.
Kampuni hiyo ya Afrika Kusini ilisitishwa baada ya kubaini ufisadi wa Sh40 bilioni zilizochotwa na Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.
Baada ya Deloitte &Touche kuzuiwa kuendelea na kazi, mwaka jana serikali mwaka jana ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutafuta kampuni ya kimataifa, kufanya ukaguzi huo kubaini ukweli.
Ofisi ya CAG iliteua kampuni hiyo ya kimataifa ya Ernst&Young, ambayo ilibaini ufisadi wa fedha hizo zaidi ya sh 133 bilioni, ambazo zilichotwa na makampuni 22.
Makampuni 13 yalijichotea sh 90.3 bilioni, ni pamoja na Bencon International LTD of Tanzania, Vb & Associates LTD of Tanzania, Bina Resorts LTD of Tanzania, Venus Hotel LTD of Tanzania, Njake Hotel &Tours LTD, Maltan Mining LTD of Tanzania.
Mengine ni Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment LTD, B.V Holdings LTD, Ndovu Soaps LTD, Navy Cut Tobacco (T) LTD, Changanyikeni Residential Complex LTD na Kagoda Agriculture LTD.
Kwa upande wa makampuni tisa yaliyochota Sh42.6 bilioni ni pamoja na G&T International LTD, Excellent Services LTD, Mibale Farm, Liquidity Service LTD, Clayton Marketing LTD, M/S Rashtas (T) LTD, Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloma and Brothers na KARNEL LtD.
Makampuni mengine mawili ambayo ni Rashtas (T) na G&T International LTD, kumbukumbu zake ikiwemo nyaraka za usajili katika daftari la Msajili wa Majina ya Makampuni na Biashara (BRELA), hazikuweza kupatikana.
Kufikia mwaka 1999 deni katika EPA lilifikia dola 623 milioni, ambazo kati ya hizo dola 325 milioni zilikuwa ni deni la msingi na dola 298 ni riba na kisha baadaye deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni.
Hata hivyo, chini ya Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme) wa mwaka 1994 kati ya serikali na Benki ya Dunia (WB), waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya fedha wanazodai, wapo waliokubali na wengine kukataa na kuongeza hadi mwaka 2004 taarifa zinaonyesha jumla ya dola 228 zililipwa chini ya mpango huo.
EPA ni akaunti ya madeni ambayo ilitumika wakati wa Mfumo wa Ujamaa, ambayo akaunti yake ilikuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) chini ya usimamizi wa BoT.
Mwaka 1985, EPA ilihamishiwa moja kwa moja BoT na ndipo mwaka juzi kulipoibuka utata wa tuhuma za ufisadi katika akaunti hiyo kwa mahesabu ya mwaka 2005/06, ambayo utata huo ulisababisha Ernst&Young kufanya ukaguzi kuanzia Septemba sita na kukabidhi ripoti yake kwa CAG mapema Desemba mwaka jana

Thursday, October 30, 2008

MANJI AZUSHIWA KIFO

Habari za kizushi zinazidi kusambaa na kuwajengea hofu mashabiki wa soka nchini hasa wa Yanga kuwa Mfadhili mkuu wa timu hiyo Yusuf Manji (kulia) ambaye amelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aghakan jijini Nairobi amefariki dunia. Blog hii ambayo nayo ilitumiwa ujumbe kadhaa juu ya kifo hicho imejaribu kufatilia kwa wadau na watu wakaribu na Maji lakini hakuna ukweli wowote hadi sasa. Kushoto ni Rais wa Yanga Iman Madega.

WATCH OUT VICTORIA !!!

David Beckham was spotted on front-row seats at an NBA game at the Staples Centre in Los Angeles yesterday.And he couldn’t keep his eyes off the Curvy Cheerleaders!!!
This not the first time David his caught feasting his eyes on the Cheerleaders,
In April, he was caught leering at a cheerleader at that same venue.
And of course Victoria made sure she was there on the next game!!!


ZULIA JEKUNDU ...RAFDA 2008




KATUNI YA LEO


P DIDDY'S TWINS

P Diddy and his adorable 2 y’old twin daughters are featured on the new issue of L’Uomo Vogue which is a men’s version of Vogue, very fashion and style driven.
Don’t they look cute???

KIAMA CHA EPA LEO


Leo ni siku ambayo Rais Jakaya Kikwete aliitangaza kuwa kiama cha wezi waliochota mapesa katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), kazi iliyokuwa ikifanywa kwa zaidi ya miezi sita na timu ya rais, kufuatilia wizi huo, imekamilika.Timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, tayari imemaliza kazi hiyo na kupeleka majalada yake kunakohusika kwa hatua zaidi.Habari ambazo tumezipata, zinasema kuwa Rais Kikwete ambaye kwa muda mrefu yuko katika ziara za kikazi mikoani, ameamua kulishughulikia suala hilo kwa uhakika ili kurejesha imani ya serikali yake ambayo imekuwa ikipakwa matope kutokana na kashfa hiyo.Watakaokumbwa na rungu hilo ni wale walioshindwa kurejesha mapesa waliyochota, ambayo ni zaidi ya sh bilioni 133, lakini pia hata wale waliofanikisha uchotaji wa fedha hizo, nao wataguswa.Vyanzo vyetu vya habari vinadai kuwa Rais Kikwete amepania kuwaonyesha Watanzania kuwa hana mzaha na mafisadi.Agosti 21 mwaka huu, wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema wazi kuwa wote waliojihusisha na wizi wa fedha za EPA, watachukuliwa hatua kali, ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani.Aidha, katika hotuba hiyo ambayo Rais Kikwete alisema fedha zitakazorejeshwa zitawanufaisha wakulima, alisema hadi Agosti tayari waliochota fedha hizo walisharejesha zaidi ya sh bilioni 53, huku wengine wakitoa ahadi ya kurejesha zaidi kufikia mwisho wa mwezi huu.Wezi wa fedha za EPA, waligunduliwa na kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa Ernest & Young, iliyopewa kazi kukagua mahesabu ya BoT na kubaini kuwa fedha hizo ziliibwa katika kipindi cha mwaka 2005/2006.Baada ya hapo, ndipo rais alipoamua kuunda timu iliyoongozwa na Mwanyika kuchunguza wizi huo.

Wednesday, October 29, 2008

WADAU WAKISEREBUKA CLUB AFRIQUE

ALICIA AKIWA NA RAFIKI ZAKE
OLIVIA NA JANINE

BRENDA NA BEV


HAWA WANAJULIKANA KAMA "THE GOODAS GIRLS"



MADADA NEYMA NA BRENDA




CELEBRITY BIG BROTHER 2009(UK)


Whitney Houston will allegedly be joined in the Celebrity Big Brother house by ex-husband Bobby Brown.
The I Will Always Love You star reportedly signed to appear in the new series of the Channel 4 show in the summer, the Daily Star claims, and now BB bosses have managed to sign her ex to the reality show too.
A source said: "It was bad enough when Bridget Nielsen had to suffer her ex mother in law Jackie Stallone turning up in the house.
"And viewers saw Rex Newmark squirm when his girlfriend Nicole arrived.
"But Bobby and Whitney together?
"It's gonna be a time bomb waiting to go off."
Whitney, 45, and R'n'B star Bobby, 39, married in 1992 but divorced two years ago after a publicly stormy relationship. The couple have a 15-year-old daughter Bobbi Kristina, 15.
Whitney has claimed Bobby was abusive to her during their marriage, and blamed him for the collapse of her career after she developed a drug addiction.
But in his autobiography, Bobby - who has confessed to cheating on Whitney - claims she drove him to drugs.
"Our marriage was doomed from the beginning," he wrote.
Celebrity Big Brother is due to return on Channel 4 in January 2009.


JULIA HUDSON SAYS SON'S SOUL IS NOW AT EASE


In the wake of losing her son, Jennifer Hudson’s sister, Julia, has now said 7-year-old Julian King’s soul is now “at ease.”
“Because I chose to do what was natural to me and love someone, it cost me my beautiful family. My wonderful, beautiful, loving, supporting mother Darnell, my true blue baby brother Jason… and last but never not least, my only son Julian, my innocent baby that was sheltered from all the evil in the world because we loved him so much,” Julia wrote in a post on her personal MySpace page

A Y !!!!!!

Anaitwa Ambwene Yessayah.Kwa wengi anafahamika kama AY huku wengine wakiendelea kumuita “Mzee wa Commercial”.Kwake muziki ni burudani na pia ni kazi.Mafanikio yake katika game ni mfano wa kuigwa na wengi hususani wasanii wanaochipukia.Ni miongoni mwa “mabalozi” wazuri wa Tanzania nje ya nchi kupitia sanaa ya muziki.Kwa mara nyingine tena mwaka huu anawania tuzo maarufu za Kisima za nchini Kenya.

WASTAAFU WA EAC WALETA KASHESHE JIJINI







VIONGOZI wa serikali, wafanyabiashara wakubwa, mabalozi na wananchi wa kawaida jana walionjeshwa ukubwa wa machungu wanayopata wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakati wazee hao walipoweka kizuizi katika eneo la daraja la Sarenda na kusababisha magari kushindwa kuingia katikati ya jiji.
Eneo hilo, lililoko makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa, ambako kuna kituo cha polisi cha Sarenda, ndio njia kuu na pekee ya magari yote kutoka maeneo ya Oysterbay, Mikocheni, Msasani na Ada, ambako wanaishi viongozi na watendaji wakuu wa serikali, mabalozi na maofisa wengine wa taasisi za kimataifa hupitia.
Maeneo ya Kinondoni, Mwenge, Kawe, Tegeta na Mbezi ambako wanaishi wananchi wa kipato cha chini na kati, pia waliathirika na mbinu hiyo ya wastaafu wa EAC kuishinikiza serikali kuwalipa mafao yao baada ya jumuiya hiyo kuvunjika mwaka 1977.
Na kutokana na maeneo hayo kuishi vigogo wengi, msururu uliozuiwa ulikithiri 'foleni' za kawaida na kusababisha watu wengi kuchelewa makazini.
Wastaafu hao wanaokaribia 200 wanataka serikali iwalipe madai yao ya fedha ambazo wanadai, ambazo ni jumla ya Sh300 bilioni.
Katika kikao chao cha juzi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, wastaafu hao walidai kuwa wangeamkia ubalozi wa Uingereza ambako walidai wangepiga kambi hadi suala lao litakapopatiwa ufumbuzi.
Lakini kiongozi wao, Nathaniel Mlaki akaeleza kuwa kabla ya kwenda ubalozini, wangepitia sehemu moja, ambayo hakutaka kuitaja na kuwahimiza wenzake kuwahi asubuhi ya jana ili waelezwe sehemu hiyo na kuwataka wabebe chupa za maji.
Baada ya kufika katika eneo hilo saa 12:20, wastaafu walilala barabarani huku wakisema maneno mbalimbali ya kuilaumu serikali kabla ya kuvua nguo baadhi yao, alisema shuhuda mmoja aliyekuwa eneo hilo wakati wa tukio.

VIKWANGUA ANGA KIBAO BANDARI YA SALAMA

Wadau angalieni jinsi jiji la bongo mambo yalivyo tambarare vikwangua anga ni vingi na vinazidi kujengwa kila kukicha miaka mitano baadaye huenda tukawa Uchina ya Afrika ya Mashariki na Kati


DEAD CELEBRITY STILL EARNING MILLIONS


Thirty years after he died aged 42, the King of Rock 'n' Roll last year pulled in $52 million (£33m), dwarfing living music stars like Justin Timberlake ($44 million or £27.5m) and Madonna ($40 million or £25m), the magazine said.
A new entry in the Forbes.com annual top-13 list at number three is 28-year-old Australian Heath Ledger, who died from an overdose of medication in January before he could collect an estimated $20 million (£12.5m) in earnings from the latest box office smash hit Batman movie "The Dark Knight," in which he played the Joker.
Forbes.com said it spoke to experts and sources inside the dead celebrities' estates and researched gross earnings, before taxes, management fees and other costs, from the period of October 2007 to October 2008 to come up with the rankings.
Elvis topped the list for a second year running due to the 30th anniversary extravaganza in Graceland -- his home in Memphis, Tennessee -- that in visitors and merchandising generated more income than his 2006 earnings of $49 million (£30.6m dollars).
Charles Shultz, who drew Snoopy and the "Peanuts" gallery of characters into existence, died in 2000 at 77. His heirs last year penned an agreement with Warner Bros. studios moving him up a notch in Forbes' list, with posthumous earnings of $33 million (£20.6m).
The father of relativity, Albert Einstein, was fourth on the list. Even though he passed away in 1955, his "Baby Einstein" toy franchise brought in $18 million (£11.2m).
American "Dr. Seuss" childrens' book author Theodor Geisel made $12 million (£7.5m) for fifth place, and Beatle John Lennon, shot dead in 1980, dropped from second to sixth place with $9 million (£5.61m).
Andy Warhol, Marilyn Monroe and actor Steve McQueen also made the top 10.
Actor Paul Newman, who died last month at 83, pulled in $5 million (£3.12m), tying with the late James Dean.
Marvin Gaye came 13th with earnings of some $3.5 million (£2.18m) thanks to interest generated by the 50th birthday of Motown Records, while Johnny Cash, who appeared on the list in 2006 thanks to the film about his career, has dropped out this year.
"For real staying power beyond the pale, the best bet is a face like Marilyn Monroe's or an attitude like James Dean's - marketers are always eager to exploit that kind of iconic fame," said the magazine

DAD STILL TO CONTROL DAUGHTERS' FINANCE

Britney Spears' personal and business affairs will be controlled by her father on a permanent basis, a court has ruled.
Britney is said to be happy that her dad stays in control of her affairs
Jamie Spears took charge of the American singer's property and finances in February following her very public meltdown.
The conservatorship, which allows him and several attorneys to control her finances, was due to end on December 31.

PANICK AS CONGO REBELS ADVANCES

Government forces are fleeing from the eastern Democratic Republic of Congo city of Goma as rebels advance, according to reports.

Congolese army soldiers and displaced civilians
Residents of the provincial capital are also leaving in panic, governor Julien Paluki added.
"People are stampeding and the city is panicking," he said.
The rebels have already overrun Kibtai, a village seven miles north of Goma that was housing at least 30,000 displaced people
Fighting between government forces and rebels loyal to General Laurent Nkunda has escalated in the past few days.
The rebels expect to be able to take Goma later today or early on Thursday, a spokesman said.
The Congo government claims Nkunda's fighters are backed by Rwandan troops. Rwanda denies the claims.
The UN's top envoy to Congo warned that its peacekeeping force in the country is stretched to the limit and needs more troops quickly.
And the UN secretary general appealed for an end to the violence.
"First and foremost, the fighting must be stopped," Ban Ki Moon said.
"And I am deeply concerned about the civilian casualties as well as increasing number of internally displaced persons."
Around 250,000 people have fled their homes since a cease-fire signed in January collapsed in August.
Nkunda claims he is fighting to protect the tiny Tutsi minority in eastern Congo.
He accuses Congo's army of collaborating with the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda, which includes Hutu militias and former Rwandan soldiers responsible for the genocide in 1994 of Tutsis and moderate Hutus

MANJI AUGUA GHAFLA

SIKU moja baada ya timu ya Yanga kuifunga Simba bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Jumapili Uwanja Mkuu wa Taifa Dar es Salaam, Mfadhili Mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa hospitali. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega, Manji aliugua ghafla juzi saa 3.30 asubuhi, wakati wakijiandaa kwenda ofisini kwake, lakini kabla ya kutoka alijisikia vibaya, ambapo alianguka na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam. "Alipofikishwa hospitali madaktari walimpima na kugundua amepatwa na malaria, ambayo ilipanda kichwani, lakini hata hivyo walimpatia matibabu na kumtaka apumzike," alisema Madega. Hata hivyo, Madega alisema baada ya Manji kupatiwa matibabu, jana asubuhi alitoka nyumbani na kwenda kutembea viwanja vya Gymkhana, akiwa peke yake kitu ambacho wasaidizi wake walimwahi na kumrudisha nyumbani kwake. Alisema wasaidizi wake walilazimika kumfuata kwa kuhofia hali yake kutokuwa nzuri, kwani bado alitakiwa kupumzika kutokana na mlolongo wa mawazo na uchovu aliokuwa nao. Madega alisema hali hiyo ilichangiwa zaidi na uchovu na mawazo yaliyotokana na mechi ya Yanga na Simba iliyochezwa Jumapili, lakini hata hivyo amewataka wana-Yanga kutokuwa na wasiwasi kwani hali ya mfadhili wao inaendelea vizuri.

XTREME PARTY

Afisa Uhusiano wa Tigo akitangaza mpambano wa DJ's na wasanii wa Afrika Mashariki utakaojulikana kwa jina la Xtreme Party utakaofanyika katika ufukwe wa Bahari ya Cine Club maalum kwa wateja wa kudumu wa Tigo kuanza kufurahia mwisho mzuri wa mwaka 2008.
Kushoto kwake ni msanii wa Bongo flava Herry Sameer (Mr Blue) na Ruta Bushoke watakaoshiriki kuiwakilisha Tanzania.
wasanii wengine watakaoshiriki mpambano huo ni kundi zima la P Unit kutoka Kenya na aliyekuwa muimbaji wa kundi la Blue 3 mwanadada Cindy.
Kwa mpambano wa DJ' atakuwepo Bush Baby na Wesley kutoka Kenya

J.HUDSON IDENTIFIES THE BODY OF HER NEPHEW

Jennifer Hudson endured more heartbreak Monday when she identified the body of her 7-year-old nephew - found shot to death in an SUV - at the Chicago city morgue. The Oscar-winning actress and singer, who grew up in the Windy City, journeyed to the coroner’s office, where the body of little Julian King lay on a gurney covered with a white sheet. “Yes, that is him,” Hudson said quietly when she saw the boy’s face on a video screen, said Sean Howard, a spokesman for the Cook County medical examiner’s office. For Hudson, whose mother and brother were found slain Friday, it brought the devastating death toll in her family to three. Still, she did not buckle under the grief: “She was just brilliant and strong,” Howard said. “Her last words to me were, ‘Just tell the general public once again to respect my family’s privacy.’”Hudson said her faith in Jesus Christ “was going to get her through that,” Howard said. “Those were her words.”As she left the facility, Hudson’s bodyguards held umbrellas to hide her anguish. Nobody has been charged with the murders, but cops are holding William (Flex) Balfour, 27, the estranged husband of Hudson’s sister Julia, at a state prison for a parole violation. “We’re following any lead we can get right now,” said city Police Superintendent Jody Weis. The Chicago Sun-Times reported Julian had been shot once in the head and was dressed in basketball shorts and a stained white T-shirt. Julian vanished Friday from his home on the gritty South Side after Hudson’s mom, Darnell Donerson, 57, and brother Jason Hudson, 29, were gunned down. Jennifer Hudson, 27, who won an Oscar for her role in “Dreamgirls,” and had remained tight with her family, immediately flew home and offered a $100,000 reward for information leading to Julian’s safe return. The hope that he was still alive was dashed Monday morning when Julian was found on the floor of a Chevy Suburban truck that had belonged to his murdered uncle.


JARIBIO LA KUMUUA OBAMA

WIKI moja ikiwa imesalia kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini Marekani, idara za usalama zimetangaza kuzima jaribio la kutaka kumuua mgombea wa urais kupitia chama cha Democrats, Seneta Barack Obama.
Uchaguzi wa rais wa Marekani umepangwa kufanyika Novemba 4 na upinzani mkali ni baina ya wagombea wa vyama vikuu viwili, Republican ambacho kinata kuendelea kushikilia madaraka kwa kumsimamisha John McCainn, na Democrats, ambacho kimemsimamisha Obama ambaye amekuwa mgombea wa kwanza mweusi wa kiti cha urais.
Uteuzi wa Obama umefanya watu wenye siasa kali za kibaguzi kukerwa na polisi imeeleza kuzima jaribio la kumuua seneta huyo wa jimbo la Illinois ambaye amekuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa Marekani.

KATUNI YA LEO


AKUDO IMPACT SOUND

Wanenguaji wa bendi ya Akudo Impact wakiwajibika wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika uzinduzi wa Wiki ya Usalama Barabarani mjini Morogoro Jumapili chini ya udhamini wa Zain ambayo ilichangia zaidi ya sh. milioni 30 kwa Wiki ya Usalama Barabarani na kupewa tuzo na kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani.

Monday, October 27, 2008

MISS EARTH "UFILIPINO" 2008

Miriam Odemba mwakilishi wa Tanzania ktk Miss Earth 2008 huko ktk Jiji la Puerto Princesa magharibi mwa visiwa vya Philippine ni mmoja wa warembo wachache wanaopewa nafasi ya kufanya vyema ktk fainali zitakazo fanyika tarehe 9, Novemba mwaka huu.




BALOZI AMALIZA MUDA WAKE SWEDEN

Mh.Balozi Ben Moses akiwa na mdau namba moja wa blogu hii malumbo jr. (kulia)pamoja na Baby
Balozi na mkewe wakiwa na wageni waalikwa
Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Hon.Dr Benn Moses amemaliza muda wake kuiwakilisha nchi yetu ,jana jioni kulikuwa na sherehe ndogo ya kumuaga iliyoandaliwa na watanzania waishio mji wa Stockholm na vitongoji(Kilimanjaro Club) ambayo ilifanyika nyumbani kwa balozi,

KATUNI YA LEO


$100,000 REWARD

Actress Jennifer Hudson is offering a $100,000 reward for the return of her nephew who vanished after her mother and brother were shot dead.
Police and the FBI are searching for clues to the whereabouts of seven-year-old Julian King - the son of Hudson's sister Julia.
The boy went missing on Friday when the bodies of his grandmother Darnell Donerson, 59, and 29-year-old uncle, Jason Hudson, were found in their Chicago home.
Hollywood star and singer Hudson offered the reward late on yesterday.
Post-mortems showed the murder victims died from multiple gunshot wounds, the Cook County Medical Examiner's Office said.
The actress identified the bodies of her mother and brother shortly after jetting back to her hometown from Florida, the Chicago Sun-Times said.
Hudson's performance in Dreamgirls earned her an Oscarfor best supporting actress in 2007.
She had been in Florida promoting her latest movie, The Secret Lives of Bees, when she was informed of the killings, according to the Chicago Tribune.
The police initially identified William Balfour, the estranged husband of sister Julia, and step-father of Julian King, as a suspect in the case.



MZEE WA UBUNTU AKIWA AMEPOZI NA SIMBA LAIVU HIVI KARIBUNI ZIMBABWE


WADAU TUPENI MAJINA YA KIKOSI HIKI ENZI HIZO


Sunday, October 26, 2008

YANGA YAIFUNGA SIMBA

Kikosi cha YANGA kilichomnyoa mnyama wa msimbazi
Ben Mwalala akichomeka mpira kimyani

UIMARA wa kipa Mzungu, Obren Curkovic, vurugu, imani za kishirikina na matukio yakiwamo ya mashabiki kurusha uwanjani chupa za maji ni baadhi ya matukio ambayo yalitawala mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyomaliza miaka karibu minane ya ubabe wa Simba dhidi ya Yanga.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa gumzo na ubishi mkubwa miongoni mwa mashabiki,Yanga imefaulu kushinda kwa bao 1-0 katika Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo uliokuwa wenye ushindani, ufundi mkubwa ikilinganishwa na mechi zinazohusisha timu hizo, Yanga walipata bao, dakika ya 15 kupitia kwa Ben Mwalala baada ya kupokea pasi ya Boniface Ambani ambaye aliwatoroka mabeki wa Simba.
Utovu wa nidhamu hasa kwa wachezaji wa timu hizo mbili kwa kiasi kikubwa uliwasababishia kadi za njano zisizopungua tano na nyekundu tatu, nusura uharibu mchezo huo mkali na mtamu ambao ulikuwa wa kuvutia, ingawa mfungaji kinara wa ligi hiyo, Ambani alibanwa zaidi na walinzi wa Simba kiasi cha kubakia kivuli.
Mussa Hassan Mgosi, ambaye alitoka kifungo cha kusimamishwa na uongozi wa klabu hiyo siku chache kabla ya mchezo huo, aling'ara na kuwa kinara akisumbua ngome ya Yanga.
Mgosi huyo huyo, pia alikosa nafasi kadhaa za kuipa timu yake mabao, zikiwamo za dakika za 23, pia 33 za mchezo huo akiwa na kipa.
Dakika moja baadaye, nahodha Nico Nyagawa akakosa nafasi nyingine ya kuwapa Wekundu wa Msimbazi bao la kusawazisha.
Kipa Curkovic, raia wa Serbia langoni aliyecheza badala ya Juma Kaseja, kulikuwa ndiyo siri ama kichocheo cha Yanga kufanya vizuri akiendeleza rekodi yake ya kutofungwa, akiwa ameruhusu bao moja pekee.
Mzungu huyo, mara kadhaa alijitosa na kuokoa mashuti kadhaa ya washambuliaji wa Simba, hasa katika kipindi cha kwanza.
Mwamuzi wa mchezo huo, Victor Mwandike aliwaonyesha kadi za njano, beki Meshack Abel wa Simba na kiungo Athuman Idd 'Chuji' wa Yanga kwa mchezo mbaya.
Haruna Moshi alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi kwa kumpiga kibao Nadir Haroub Cannavaro akidai alikuwa amemchezea rafu ya kumrukia, jambo ambalo lilimkasirisha.
Dakika ya 76, mwamuzi aliwatoa nje kwa kadi nyekundu, Meshack Abel na Mwalala baada ya kutishiana kuzipiga ngumi.
Kipindi hicho, Simba iliwatoa Gabriel na Nyagawa na kuwaingiza Ulimboka Mwakingwe na Mohammed Kijuso.
Yanga nao waliwapumzisha Ngassa na Chuji na kuingia Castory Mumbala na Kigi Makassy.
Hata hivyo, Mwandike alimpa kadi ya njano, Emmanuel Gabriel kwa kujiangusha kwa makusudi katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Matukio
Naye Vicky Kimaro anaripoti kuwa, Simba waliingia uwanjani muda wa saa 8.45 mchana kwa mbwembwe huku Mgosi akiwa wa kwanza kushuka kutoka katika gari aliingia uwanjani akifuatwa na mwenyekiti, Hassan Dalali.
Wawili hao walikwenda hadi kona ya kaskazini mwa uwanja wakifuatwa na kundi zima la wachezaji, wanachama wa kundi la Friends of Simba ambao wanataka kuingia uwanjani, lakini wakazuiwa na wanausalama.
Yanga kwa upande wao waliingia uwanjani saa 9.00 wakiongozwa na winga Mrisho Ngassa na kwenda hadi katikati ya uwanja, akainama na kushikana paji la uso akifuatiwa na wenzake.
Katika kipindi cha kwanza, mashabiki wa Simba wanataharuki na kuanza kurusha chupa za maji uwanjani wakipinga kitendo cha mwamuzi Mwandike kupeta baada ya wachezaji wao watatu kufanyiwa madhambi.
Nje ya dimba, mashabiki nao walijaribu mara kadhaa kurushiana ngumi za hapa na pale, ingawa askari walikuwa macho kutuliza rbasha hizo ikiwamo kutumia mabomu ya machozi kutawanya mashabiki waliojaribu kuingia uwanjani uliokuwa umesheheni mashabiki na tiketi kumalizika.
Matukio ya imani za kishirikina nayo pia yalichukua sehemu ya mchezo huo baada ya Mgosi, dakika ya 69 kwenda katika lango la Yanga, kufukua na kuondoka na kitu kinachodaiwa kuwa hirizi.
Mgosi alitupa kitu hicho nje ya uwanja ambako shabiki mmoja alikiokota na kwenda nacho upande walikokuwa mashabiki wa Simba.
Kitendo hicho kilimzawadia kadi ya njano Mgosi. Tukio hilo linachafua hali ya hewa uwanjani kwa wachezaji kuonyeshana ubabe, kurushiana ngumi.
Mashabiki wa Simba wanafanya vurugu zikiwamo za kurusha chupa za maji kuelekea kwa wachezaji wa Yanga na mwamuzi huyo huku wakimlaumu kuwa aliwabeba kwa kiasi kikubwa wapinzani wao.
Mwakingwe, ambaye aliifunga Yanga mwaka jana katika Ligi Ndogo aliangua kilio baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi huyo.
Kwa upande wa Yanga ni nderemo, vifijo na nyimbo mbalimbali zikieleza kuwa zama za uteja kwa Simba basi!
Kocha wa Yanga, Dusan Kondic alieleza kufurahishwa na mchezo,pia matokeo akieleza kuwa ameibadili historia mbaya ya timu yake kufungwa na Simba.
Alieleza kuwa ushindi huo umechangiwa na wachezaji wake ambao walicheza bila shinikizo.
Mwenzake wa Simba, Krasimir Bezinski alieleza kuwa timu yake imecheza vizuri kuliko Yanga, lakini washambuliaji wake ndio waliomwangusha kwa kukosa umakini.