Kimbembe hicho kilitokea usiku wa kuamkia jana, eneo la Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam, jirani kabisa na Saluni ya kiume ya B. Table, pembeni mwa Ukumbi wa Lango la Jiji, ambapo Kanumba alifika hapo kwa lengo la kunyoa na kutengeneza nywele zake.Inaelezwa kwamba, muda mfupi baada ya Kanumba kuingia ndani ya saluni ya B. Table, Wema ambaye ni Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, alitinga eneo hilo akiwa na wapambe wake, ambapo alimuomba Kanumba atoke nje kwa lengo la kufanya mazungumzo ya muda mfupi.Bila hiana, Kanumba alitii wito wa aliyekuwa mpenzi wake huyo, ambapo alipofika nje, alipigwa na butwaa kuona timu ya wapambe wa Wema waliokuwa wakimsubiria kwa ‘hamu’.Kabla ya mazungumzo hayo kuanza, Wema alianza kuporomosha matusi ya nguoni yasiyoandikika huku akiungwa mkono na aliyetajwa kwa jina la Asha Jumbe ambaye ni wifi yake Wema kwa mwanaume mwenye uhusiano wa kimapenzi na mnyange huyo kwa sasa.Katika kuonyesha kwamba walikuwa wamedhamiria kumpa jamaa kipondo, Wema na wapambe wake ‘wakimkwida’ Kanumba na kumvuta shati alipokuwa akiwakwepa na kuingia saluni kwa nia ya kukimbia shari.Waliposhindwa kumpa kichapo, Wema na wapambe wake waliamua kuvunja kioo cha gari la Kanumba aina ya RAV 4 kwa kutumia ‘shoo’ ya gari hilo ambayo tayari walikwishaivunja kwa kutumia mawe kwa lengo la kuitumia kama silaha.Kitendo kile kilimuudhi sana Kanumba na kumsabishia hasira kali kabla ya kutoka nje ya saluni hiyo akiangua kilio kwa nia ya kumvaa Wema ili amshikishe adabu, lakini aliamuliwa na wafanyakazi wa saluni hiyo.Hata hivyo, Wema na wenzake walipoona ‘soo’ linakuwa kubwa waliamua kutimka na kutokomea kusikojulikana.Baadaye Kanumba aliamua kwenda kuripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Magomeni na kufungua Jalada la Kesi namba MAG/RB/1923/2009, ambapo sasa Wema anasakwa na polisi.Mmoja wa askari aliyekuwa zamu kituoni hapo juzi usiku ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, alithibitisha kutokea kwa tukio.
No comments:
Post a Comment