.

.

.

.

Sunday, February 01, 2009

ISSA MICHUZI AMPONGEZA KIKWETE


Globu ya jamii(http://www.issamichuzi.blogspot.com/ ) inapenda kumpa pongezi JK kwa kuwashushua viongozi wa jiji la Dar kwa tabia yao ya kuwanyima raha wakazi wake kwa kupanga matumizi ya sehemu wazi wanavyojua wao.
Globu hii, ambayo ilikuwa mstari wa mbele kukemea hayo, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa wadau wasiende kwenye fukwe kama pale Aga Khan kupiga picha, imefurahishwa sana, sana kwa mshushuo huo wa uhakika.
Sijui hawa viongozi wa jiji hili wana tatizo gani. Globu hii inadhani wana utindio wa ubunifu kwani kama ingekuwa vinginevyo mambo yangekuwa mswano kila mahali.
We fikiria unazuiwa kwenda bichi, bustani ya Mnazi Mmoja imepigwa kufuli saa zote, na zingine kama za pale Magomeni, Temeke, Mwananyamala na kweingineko hata hazitamaniki. haishangazi kukuta kila mtu anaelekea Coco Beach kila siku ya mapumziko kutokana na unoko wa viongozi wa jiji.
JK wala hakuwalazia damu. Aliwataka madiwani hao wa jiji hili (hata sijui wanafanya kazi gani) kuhakikisha kuwa viwanja vya Jangwani vinabakia kuwa vya matumizi ya umma hasa michezo na sio vinginevyo.
JK aliyasema hayo wakati akizungumza na madiwani wa Jiji la Dar es Salaam katika viwanja vya Karimjee hivi karibuni.
Alisema kumekuwa na tabia ya mamlaka za Jiji kuvamia viwanja vya wazi vilivyotengwa kwa ajili ya michezo na kutoa mfano wa viwanja vya Jangwani, akishangaa magari ya mizigo yakiwa yameegeshwa eneo hilo.
Alisema mwanzo alifikiri magari hayo yamevamia eneo hilo, lakini baadaye alikuja kufahamu magari hayo yalielekezwa na mamlaka husika kuwa hapo, ambapo alisema uamuzi huo haukuwa wa haki.
“Tafadhali tafuteni mahala pengine pa kuegesha magari yenu na viacheni viwanja hivyo kwa ajili ya watu kufurahi na kucheza, mji uliopangwa vizuri ni lazima uwe na mahali palipotengwa kwa ajili ya michezo.
“Nakumbuka enzi zetu nilikuwa natembelea maeneo ya Gerezani kwa ajili ya mchezo wa mpira wa kikapu, ambapo ilikuwa ni muda mwafaka kwa vijana kufurahi na kubadilishana mawazo,” alisema.
Pia JK alishangaa kusikia kuwa mamlaka zinawakataza wananchi kutembelea maeneo ya fukwe hasa wakati wa sherehe za harusi.
Alisema hakuna cha kupoteza kama wahusika wataenda kwenye fukwe hizo na kupiga picha kwa muda mfupi katika matukio yao muhimu na kwamba kinachotakiwa si kuwazuia, bali kuweka utaratibu maalumu.
Pia alisema fukwe hizo zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama zitatunzwa vyema.
Leo nimepita hapo bichi ya Aga Khan nimekuta hakuna tena yale mabango ya kukataza watu wasile raha sehemu hiyo. Yaani hadi raha.
Ila hapa cha kujiuliza; hivi ni hadi JK aache shughuli za maana za kitaifa na kimatifa aje awafunze kazi madiwani????
Wadau hii imekaaje?
-MICHUZI

1 comment:

  1. Kwakweli JK anahitaji viongozi wenye ari kama yake na sio hao wasioelewa kazi zao, Ila nakumbusha kua kuna vijana wengi wanaweza ila tupewe nafasi. to be honest asilimia 90 ya viongoziwa Tz hawana lolote na hawajui kazi, Kiongozi ni JK,LOWASA,MAGUFULI,Makamba,Mwaibula na Kandoro hao wanafanyakazi. Viongozi wengine wanachofanya ni kukurupuka na kujilimbikizia mali kwa manufaa binafsi. kweli KIONGOZI anaamka na kutoa amri kua watu wasiende bichi na viwanja vingine JE! HUYO NI KOIONGOZI au tahira? Hata aibu hawana? Enzi za MWALIMU na LOWASA walikua wanachapwa kwa uzembe wao wakutokufikiria

    ReplyDelete