.

.

.

.

Saturday, February 21, 2009

ALBINO WA KANADA AANZISHA MAPAMBANO


Raia wa Kanada mwenye ulemavu wa ngozi- Albino, Peter Ash na wawakilishi wawili wa kampuni yake ya hisani aliyoianzisha mwaka jana baada ya kusikia mauaji hayo wameandamana makao makuu ya Umoja wa mataifa nchini Marekani kulaani mauaji hayo.

Peter Ash alisema kwamba alianza kusikia habari za kuuliwa kwa albino Tanzania na kunyofolewa kwa baadhi ya viungo vyao mwaka jana.Ash alisema kwamba katika kipindi cha miaka miwili uvumi umeenea katika ukanda wa Afrika Mashariki kwamba vinywaji vinavyochanganywa na damu ya albino, viatu vinavyotengenezwa na ngozi ya albino na sehemu ya viungo vyao zinapowekwa kwenye nyavu za kuvulia samaki huleta utajiri.Ash alisema kwamba alishtushwa zaidi aliposikia kwamba waganga wa kienyeji walimwambia mtangazaji wa BBC aliyejifanya mfanyabiashara anayetafuta utajiri kwamba wanaweza wakamletea mwili wa albino kwa dola 2,000.Zaidi ya albino 40 wameishauliwa tangia mwaka 2007, baadhi yao mbele ya familia zao na makundi ya vijana ambayo baada ya kuwaua albino hao hukata na kuondoka na viungo vyao kama vile sehemu za siri, miguu na vichwa vyao.Mwaka jana Bwana Ash alizindua kampuni ya hisani iliyoitwa Unde the Same Sun ili kusaidia mapambano ya kupinga mauaji ya Albino nchini Tanzania na kuishinikiza serikali ya Tanzania kuongeza jitihada zaidi za kutokomeza mauaji hayo.
Mwezi huu Ash akiwa na wawakilishi wake wa Tanzania Josephat Torner na Samwel Mluge ambao wote ni Albino waliandamana hadi makao makuu ya umoja wa mataifa kuutaka Umoja wa Mataifa uishinikize serikali ya Tanzania kuunda tume maalumu ya kuchunguza mauaji ya albino Tanzania.
Ash na wenzake walisema kwamba hadi sasa zaidi ya watu 170 wameishakamatwa kutokana na mauaji ya albino Tanzania lakini hakuna hata mmoja aliyepelekwa mahakamani.Pia wamelitaka jeshi la Tanzania kushiriki katika kuzuia mauaji hayo kwakuwa hawaliamini jeshi la polisi kutokana na baadhi ya maafisa wake kuwa miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa.

No comments:

Post a Comment