.

.

.

.

Sunday, February 22, 2009

BAADA YA KIFO CHA MWANAYE AKUTWA AMEJINYONGA


SAMAHANI KWA PICHA HII YA HUZUNI

Kijana mmoja aliyefahamika kwa Dismas Tarimo (36), mkazi wa Shimo la Udongo Kurasini, jijini Dar es salaam, amekutwa amejinyonga kwa kutumia shati lake na mkanda wa suruali katika makaburi yaliyopo Shimo la Udongo juzi saa sita usiku.Ilielezwa na mmoja wa ndugu wa karibu wa marehemu kuwa chanzo cha Tarimo kuamua kujinyonga ni tofauti ya mawazo iliyojitokeza na wanafamilia wenzake juu ya mazishi ya mwanawe Baraka Tarimo (3) aliyefariki kwa ugonjwa wa ‘Nimonia’. Tarimo alitaka mwanawe asafirishwe akazikwe kwao kijijini lakini ndugu walitaka wazike jijini Dar, kwa hasira Tarimo aliamua kwenda makaburini na kujitoa uhai akiamini hakutendewa haki na ndugu zake.

1 comment:

  1. Ninaona kutoka msiba mmoja amatengeneza miwili, ninatumaini angalau yeye alipata nafasi ya kuzikwa huko kijijini!

    ReplyDelete