.
.
Wednesday, February 04, 2009
BIMA YAACHISHA KAZI WAFANYAKAZI WAKE WOTE
Wafanyakazi wote wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wameachishwa kazi na kulipwa mafao yao kuanzia jana ili kupisha mpango wa kuliboresha shirika hilo litoe huduma kwa ufanisi. Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya NIC, Dk. Hamis Kibola jana, ilisema kuwa shirika hilo litaajiri wafanyakazi wapya kulingana na mahitaji ya shirika. Dk. Kibola alisema leo na kesho shirika hilo halitatoa huduma ili kupisha kazi ya kuajiri upya na huduma itarejea tena Jumatatu ijayo wakati mchakato wa kuajiri utakapokuwa umekamilika. Inakadiriwa wafanyakazi 500 wataachishwa kazi na shirika hilo litaajiri wafanyakazi wachache wenye ufanisi na wanaoweza kuleta changamoto mpya ya kulifanya shirika hilo liwe na tija na kuhimili ushindani wa biashara ya bima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment