.

.

.

.

Tuesday, February 17, 2009

CHAMELEONE AIBUA ALBUM MPYA

Mwanamuziki Mkongwe Nchini Uganda, Jose Chameleone aliushangaza umati wa watu waliofurika kushuhudia uzinduzi wa Album yake mpya ya BAYUDA pale walipoweza kuimba akiwa kwenye kiti cha matairi kutokana na ajali ya kuanguka toka ghorofani aliyoipata mwaka jana Jijini Arusha.Akiimba na kushangiliwa na umati wa watu waliojitokeza kwenye uzinduzi huo Chameleone alionyesha kuwa pamoja na ajali hiyo yeye kama msanii asingeweza kushindwa kuwaburudisha washabiki wake pale kila mmoja aliyehudhuria show hiyo alipokubali kuwa jamaa anitisha.Jose Chameleone alipata ajali ya kuanguka toka ghorofani mjini Arusha ambapo alikuja kutumbuiza kwenye show ya Fiesta Jijini humo.Akiongea kwa furaha mara baada ya show hiyo Chameleone aliweza kuwashukuru wapenzi na washabiki wake wote kwa kujitokeza katika uzinduzi wa album hiyo."Nafurahi kwa moyo mmoja naamini bila nyie nisingeweza kuwa hapa, ni album yangu ya 11 toka niingie kwenye game na naamini bado mnanipenda, kuonyesha ni jinsi gani nakubali" alisema Chameleone.

No comments:

Post a Comment