.

.

.

.

Tuesday, February 17, 2009

MH.MASHA AVUNJA UKIMYA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha jana alivunja ukimya dhidi ya tuhuma zinazomwandama kuwa aliingilia mchakato wa zabuni ya mradi wa uchapishaji vitambulisho vya taifa, alipokanusha kuwa na uhusiano wowote na kampuni ya Sagem Securite na kusema kuwa yuko tayari kujiuzulu iwapo itathibitika kuwa alifanya kosa hilo au alipokea rushwa.
Waziri Masha pia alisema kuwa taarifa za vyombo vya habari kuwa alikuwa nchini Uswisi Oktoba mosi kuzungumzia tenda hiyo, si sahihi na kuonyesha nyaraka za kusafiria zinazoeleza kuwa siku hiyo alikuwa akitokea Hong Kong kuja Tanzania.
Masha ameibuka kuzungumzia tuhuma zake siku moja baada ya Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutaja kampuni sita zilizopita ngwe ya kwanza ya mradi huo uliotengezewa zaidi ya Sh200 bilioni, huku Sagem Securite ikiwa imetupwa nje ya mchakato.

No comments:

Post a Comment