.

.

.

.

Sunday, February 15, 2009

RAIS JK AFANYA UTEUZI MPYA

Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, amemteua Brigedia Jenerali Samwel Kitundu kuwa Mkuu mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Rais Kikwete pia amempandisha Cheo Brigedia Jenerali Kitundu kuwa Meja Jenerali kuanzia Februari 9, mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Uhusiano Makao Mkuu ya Jeshi, ilisema kuwa Meja Jenerali Kitundu, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenerali Mstaafu Martin Madatta ambaye alistaafu utumishi jeshini Septemba, mwaka jana. Kwa uteuzi huo, Meja Jenerali Kitundu anashika nafasi ya juu kabisa katika Jeshi la Kujenga Taifa lenye jukumu kubwa la malezi ya vijana na uzalishaji mali. Meja Jenerali Kitundu anakuwa Mkuu wa tisa wa JKT tangu jeshi hilo lianzishwe mwaka 1963. Wakuu wengine walioongoza Jeshi hilo ni pmaoja na R S Kaswende, David Nkulila, Laurence Gama, Meja Jenerali Nelson Mksisi na Meja Jenerali Makame Rashid. Makamanda wengine waliowahi kuongoza Jeshi hilo, ni pamoja na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye ni Mkuu wa sasa wa Mjaeshi, Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa sasa wa JWTZ na Meja Jenerali Mstaafu Martin Madatta.

No comments:

Post a Comment