.

.

.

.

Monday, February 23, 2009

TAIFA STARS YALALA 1-0


BAO lililofungwa kwa kichwa na Traore katika dakika ya 35 katika mchezo wa jana, limeiwezesha Senegal kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Tanzania katika mchezo wa michuano ya CHAN.
TRAORE alifunga bao hilo akiunganisha krosi safi kutoka upande wa kulia wa Uwanja baada ya mabeki wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Said Swed wakiwa wameduwaa.Licha ya kufunga bao hilo katika mchezo huo wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), Stars ilionekana kuwamudu Senegal hasa katika dakika za mwanzo na mwisho za pambano hilokali na la kusisimua.Mshambuliaji wa Stars, Jerry Tegete alikosa bao la wazi katika dakika ya nane ya mchezo huo baada ya kupiga shuti kali kuelekea langoni kwa Senegal, lakini mpira huo uliwababatiza mabeki.Dakika nne baadaye, Mrisho Ngassa alipiga krosi safi kuelekea langoni kwa Senegal lakini haikuweza kuunganishwa na washambuliaji wenzake kutokana na kutokuwapo katika eneo la hatari kwa mchezaji yeyote wa Stars.Bao hilo la Senegal lilidumu hadi mapumziko licha ya Kocha wa Stars, Marcio Maximo kuwatoa Bonny na Haruna Moshi ‘Boban’ katika kipindi cha kwanza na nafasi zao kuchukuliwa na Nurdin Bakari na Mussa Hassan ‘Mgosi’.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini hakuna timu iliyoweza kupata bao japokuwa kila wakati safu za ushambuliaji za timu hizo ziliweza kufika katika lango la wapinzani wao.Stars itashuka tena uwanjani keshokutwa kucheza na wenyeji Ivory Coast ambao katika mchezo wa ufunguzi walifungwa mabao 3-0 na Zambia. Stars iliwakilishwa na; Shaaban Dihile, Shadrack Nsajigwa, Juma Jabu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Swed, Geofrrey Bonny, Haruna Moshi ‘Boban’, Henry Joseph, Nizar Khalfan , Mrisho Ngassa na Jerry Tegete

No comments:

Post a Comment