Serikali imebaini kuwapo mpango mchafu wa kutaka kuvuruga ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon nchini, imeelezwa.Akizungumza jana Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema kuna kundi la watu wanaojiita 'Wazee wa Pemba' linapanga siku hiyo kuingilia ratiba ya mgeni huyo na kufanya maandamano. Katibu Mkuu wa UN anatarajia kufanya ziara kuanzia kesho hadi Jumamosi, kutokana na mwaliko aliopewa na Rais Jakaya Kikwete walipokutana New York, Marekani, Septemba mwaka jana. Waziri alisema baada ya Serikali kulibaini hilo, hivi sasa inalifanyia kazi ikiwa ni pamoja na lile la wapinzani wa Ba Ki-moon kutoka nje ya nchi, wanaopanga kutumia baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari mbaya kumhusu."Ombi letu ni kuhakikisha watu hao hawafanikiwi katika azma yao ya kutumia vyombo vya habari vya hapa nchini kuandika mambo mabaya ya kumchafulia jina mgeni wetu," alisema Waziri Membe.
No comments:
Post a Comment