.

.

.

.

Thursday, March 26, 2009

MALECELA ALONGA

Mwanasiasa mkongwe, John Malecela, ametaka malumbano ya kisiasa yanayoendelea sasa kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakome mara moja na hayana msingi katika maendeleo ya nchi. Malecela (75), ambaye ni Mbunge wa Mtera (CCM) pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, aliyasema hayo Dar es Salaam jana.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Sea View, Malecela alisema si vyema wala busara kuendesha malumbano kupitia vyombo vya habari ilhali kuna mamlaka zinazohusika. “Kama mwanasiasa wa kawaida na Mtanzania, ningependa kusema kuwa malumbano haya katika vyombo vya habari, ningeomba yakome, maana hayawasaidii Watanzania,” alisema Malecela.

Aliwataka wahusika katika malumbano hayo ambayo hata hivyo hakuwataja kwa majina, watumie vyombo husika kuwasilisha hoja zao. Alisema ni vyema kila jambo likapelekwa katika chombo husika, ambavyo ni vyama, Bunge na serikali ambako yatashughulikiwa ipasavyo na si kuwachanganya wananchi. Malecela alisema malumbano haya huchangiwa na vyeo, fedha na mambo mbalimbali waliyonayo wanaolumbana.

No comments:

Post a Comment