.

.

.

.

Thursday, March 26, 2009

MGAO WA UMEME WAANZA BONGO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza rasmi mgawo wa nishati hiyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kupungua kwa ufuaji wa umeme kwa megawati 50. Taarifa iliyotolewa leo na Tanesco, ilisema mgawo huo wa muda utakuwa ni wa kila siku kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana na saa 12 jioni hadi saa 4 usiku.

Hali hiyo, taarifa ilisema imechangiwa na kusimama kwa mitambo miwili katika kituo cha Songas (UGT1 na UGT5) ambacho kwa kawaida huzalisha megawati 53. Mmoja unafanyiwa ukarabati wa kawaida na mwingine umeharibika. Ilisema usambazaji umeme kwa Dar es Salaam na Zanzibar unategemea nishati hiyo kutoka mitambo ya nguvu za maji na mtambo wa gesi wa Ubungo kupitia transfoma namba T6 na T7. Ziada ya hapo, wazalishaji umeme binafsi ikiwa ni pamoja na Songas wanaongeza nishati hiyo kwa Dar es Salaam sambamba na transfoma hizo.

No comments:

Post a Comment