.

.

.

.

Friday, March 27, 2009

POLISI YAMSHIKILIA MH.CHENGE




Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge anashikiliwa na polisi kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya wasichana wawili usiku wa kuamkia leo sehemu za oysterbay jijini dar, kamanda wa kanda maalum ya mkoa huu afande Suleiman Kova,amethibitisha
Afande Kova amesema kwamba Mh. Chenge alikuwa akiendesha Toyota Pick-UP Hilux yenye usajili namba T 512 ACE ambayo iligongana na Bajaji yeney namba za usajili T 736 AXC na kusababisha vifo vya hao wasichana wawili ambao hadi sasa hawajaweza kutambulika.
Amesema marehemu walikuwa wamekodi Bajaji na kwamba dereva wao alinusurika na hadi sasa hajulikani aliko na anatafutwa.
Afande Kova kasema Mh. Chenge ataendelea kushikiliwa wakati upelelezi unaendelea chini ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya jinai Afande Peter Kivuyo.

Afande Kova alimtaja mmiliki wa bajaji kuwa ni Bi. Zuwena Faith ambaye ameamriwa kuripoti polisi, ikiwa ni mojawapo ya hatua za kusaidia upelelezi wa kumsaka dereva wa bajaji aliyeingia mitini.
Miili ya marehemu, ambao wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 na 28 imehifadhiwa mochuari ya hospitali ya mwananyamala.

No comments:

Post a Comment