.

.

.

.

Thursday, March 05, 2009

WEMA SEPETU ATOKA RUMANDE MAMA YAKE AJA JUU

Wema akibebwa Kindava na Mama yake baada ya kutaka kuondoka na "mumewe" Jumbe ambaye familia yake haimtambui.
"Nakwambie twende nyumbani haraka kama sivyo ninakufutia dhamana yako sasa hivi ili urudishwe rumande haraka huyo Jumbe si hatumtambui na kama anakupenda mbona hajakudhamini?” Mama Wema.
“ Mimi labda nife ndio mwanangu ataolewa na kijana huyo sitaki hata kumuona kwa kuwa kwanza ndio chanzo cha mwanangu kuharibika, lakini hata hivyo mimi naona kama alikuwa na nia na mwanangu mbona hata dhamana hakuja kumtolea dhamana” aliendelea kufoka Mama kwa hasira.
Picha ya juu Wema akiingia mahakamani toka mahabusu na ya kati akiwa ndani ya mahakama na mshitakiwa mwenzake Asha Jumbe.




Wema Sepetu akipewa pole na Yusuf Jumbe (Aneyedaiwa mumewe) baada ya kuachiwa kwa dhamana leo Mahakamani Kinondoni akikabiliwa na shitaka la kuharibu gari la mwigizaji Steve Kanumba.
Mrembo huyu aliyepata kuwa miss Tz alikuwa rumande toka wiki iliyopita baada ya kukosa dhamana .



No comments:

Post a Comment