George Mshana (30) anayedaiwa kumbaka mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka mitatu (jina linahifadhiwa) amepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kusomewa mashitaka yake.
Akisoma mashitaka hayo, mwendesha mashitaka Inspekta wa Polisi Nassoro Sisiwaya, mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo, Emelius Mchauru, alidai kuwa mnamo Aprili 16, mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika kituo cha mabasi Mwenge , Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Mshana alimbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu ndani ya Daladala. Hata hivyo Mshana alikana tuhuma hizo na kutupwa tena rumande baada ya wadhamini wake kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo ilipigwa kalenda hadi Mei 5 mwaka huu.
Mshana anadaiwa kumbaka mtoto huyo baada ya kumuomba kutoka kwa mama yake ili amsaidie kumpakata ndani ya daladala, ambapo ilidaiwa alimkalisha mapajani na kuanza kumvua nguo ya ndani ya siri kisha na yeye kufungua zipu na kujipaka mafuta kwenye uume wake na kuanza kufanya jaribio la kumuingilia binti huyo.
Hata hivyo wakati akifanya jitihada za kumuingilia ilidaiwa kuwa, mtoto alianza kupiga kelele za maumivu, zilizomshitua mama yake na ndipo ilipobainika kuwa binti yake alikuwa anaingiliwa!!!
No comments:
Post a Comment