.

.

.

.

Wednesday, April 29, 2009

SHEREHE ZA MUUNGANO LONDON

Mheshimiwa Balozi, akiwa na Maofisa wengine wa Ubalozi, baada ya kumalizika kwa Ibada ya kuiombea Nchi yetu Tanzania.
Ibada hiyo uandaliwa kila Mwaka na Kanisa la Westminister Abbey inapofika siku ya Muungano. Kanisa la Westminister Abbey huandaa Ibada kwa Kila Nchi Mwanachama wa Commonwealth zinapofika siku za nchi zao Mataifa yao. Kulia mwa picha ni Bwana David Nginilla, Bwana Amos Msanjila, Mh. Balozi, Mama Mwanaidi. S. Maajar, Dada Caroline Chipeta, na Bwana Clement Kiondo.
Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi S. Maajar {Pili Kushoto}, akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania kwenye Sherehe za kuadhimisha Miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Toka kulia mwa picha ni Mh. Abubakar Faraji, Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania hapa Uingereza, Bwana Katega-Muwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, Bwana Maina- Mwenyekiti wa CCM Reading, Bwana Jackson- Mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, na Bwana Fredy {nyuma ya picha}- Mtanzania na Mtangazaji kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC-London

No comments:

Post a Comment