NI dhahiri mashabiki wa Yanga walikuwa wanalitambua kwamba timu yao haiwezi kushinda, mabao 4-0 lakini walichokifuata ni kuona aina ya soka ya Al Ahly na nyota wake.
Al Ahly iliifunga Yanga mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika mjini Cairo, ikaifunga tena bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni ikiwa ni mchezo wa marudiano.
Yanga ambayo iliweka rekodi kwa kuitoa Etoile d’Or Mirontsy ya Comoro kwa mabao 14-1 walishindwa kabisa kuonyesha soka yao halisi huku Al Ahly wakionana karibu kila idara katika vipindi vyote.

No comments:
Post a Comment