Akiongea na Uwazi hivi karibuni juu ya viumbe hao alisema kuwa alianza kumsumbua tangu Januari, 2002.Akieleza mkasa huu wa kusikitisha, kijana huyu anasema kwamba, matukio haya ya kusikitisha humtokea wakati akiwa amelala usiku, ambapo mara tu aanzapo kusinzia humuona mtu au watu wakimfuata kitandani na kumvua nguo kisha kumfanyia mambo ya aibu.
Kijana huyo alisema kuwa , wakati afanyiwapo vitendo hivyo hupatwa na maumivu makali kupita kiasi, mwili wote humlegea, hutokwa na jasho jingi mwilini, na ubongo wake hushindwa kufanya kazi kwa muda na mara nyingi hupotelewa na fahamu kwa muda wa kama robo saa hivi na kisha baadaye fahamu zake zinapomrudia ubongo wake huwa umechoka sana huku ukishindwa kufanya kazi vyema.
Kutokana na kufanyiwa vitendo hivyo kwa muda mrefu, imefikia kipindi uanaume wake umepungua, mishipa inayozitawala sehemu zake za siri imelegea na kushindwa kuzuia vyema haja kubwa, kwa upande wa masuala ya mahaba, kijana huyo amedai ameshapoteza uwezo wake wa kulala na mwanamke.“Kutokana na kufanyiwa unyama huu, baadhi ya sehemu zangu za mwili zimekwishaathirika ikiwa ni pamoja na sehemu zangu za siri ambazo zimeshalegea kabisa, hazifanyi kazi, nimekuwa kama mwanamke, ni mwanaume ukiniona lakini hakuna kitu wala sifanyi chochote,” anaeleza Magesa kwa masikito makubwa.Kwasababu ya muendelezo wa vitendo hivyo, imekuwa ikifikia hatua ya kijana huyu kuchanganyikiwa na kwamba anaona heri kufa kuliko kuendelea kuishi duniani kwa mateso.
Katika hali ya kutafuta suluhisho la matatizo yake, amejaribu kuomba ushauri kwa marafiki na jamaa zake wa karibu, pia, baada ya mambo kuzidi, aliamua kugeukia upande wa dini, ambapo aliamua kuokoka na kwenda kwenye maombezi mbalimbali ya walokole lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda.“Watu wengi walinishauri niende kwenye maombi mpaka sasa sijapata nafuu yoyote ile, nimejaribu kulala na watu wengine wakubwa kwa umri ili wanipe ulinzi niwapo kitandani lakini bado matatizo haya yanaendelea kwani mara zote wamekuwa wakidai hawaoni chochote mbali na kusikia mimi nikilalamika usiku kucha.“nimekwenda sehemu mbalimbali wafanyazo maombi: viwanja vya shule za msingi, vituo vya mabasi, kanisani, karibu na uwanja wa ndege Musoma, nimeombewa nyumbani kwa nyakati mbalimbali, bado hali haijawa nzuri, nimeshakata tamaa ya maisha na nimeona heri niende kwenye dawa za asili,” alisema kijana huyo.
Jambo ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa kijana huyo kupata tiba za asili kwa urahisi ni uwezo wake wa kifedha, ingawa mwenyewe anasimulia kwamba kuna watu anaowajua ambao walishawahi kupatwa na matatizo kama yake lakini baada ya kuzunguka kwa waganga wa jadi walifanikiwa kupona.Magesa anasikitishwa sana na hali anayokumbana nayo na kufikia kipindi anaona kwamba ufukara wake kama kikwazo kikubwa cha yeye kupata suluhisho la matatizo yake.“Mheshimiwa kama maombi yameshindwa kunipa nafuu nifanyeje? Niendelee kuumia na kuishi kwa mateso na hali tiba zipo, au niendelee kuteseka kwasababu ya ufukara nilionao, hivi mimi niliumbwa niteseke kwa ajili ya ufukara?” Alihoji Magesa.
Kijana huyu anaomba msaada wa hali na mali ili aweze kutafuta tiba ya matatizo yanayomkabili, kutokana na maelezo yake kiasi cha shilingi laki moja na nusu (150,000/=) ndicho kinachohitajika kutatua tatizo lake.
SOURCE : UWAZI
No comments:
Post a Comment