Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, amesema kama mkataba wa kukusanya ushuru katika Kituo Kuu cha Mabasi Ubungo (UBT) ni mbovu ambao kampuni ya familia yake inahusika nao, basi wa kulaumiwa ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Kampuni ya Smart Holdings ambayo ina uhusiano na mwenasiasa huyo iliingia mkataba na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kukusanya mapato kituo hicho cha mabasi yaendayo mikoani.
Hata hivyo, mkataba huo ulizua utata baada ya kubainika kuwa una harufu ya ufisadi, jambo lililoifanya serikali kuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuanza kufanya ukaguzi
No comments:
Post a Comment