.

.

.

.

Monday, May 25, 2009

PAROKO AMPA UJAUZITO MWANAFUNZI

Katika hali inayoonekana kuwashitua wengi, mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Farkwa amemtaja Paroko wa Parokia ya Farkwa, Padri Godian Simpinge, kuwa ndiye aliyempa mimba.
Tukio hilo lilikuja baada ya wanafunzi wawili wa sekondari hiyo, mmoja wa kidato cha kwanza na mwingine kidato cha tatu kukutwa na ujauzito, kufuatia zoezi la upimaji wa mimba lililoendeshwa na shule hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mkuu wa shule hiyo, Rajabu Yengela, alisema zoezi hilo lilifanyika Aprili 22 mwaka huu. Alisema mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne ambaye naye alihisiwa kuwa na ujauzito alitoroka wakati wa zoezi hilo likiendelea.
Mwalimu Yengela alisema mwanafunzi wa kitado cha kwanza alikutwa na ujauzito wa miezi sita, huku mwenzake akiwa na miezi minne toka apate ujauzito.
Mwalimu Yengela alisema, baada ya matokeo hayo, bodi ya shule iliagiza wanafunzi wote waitwe ili waeleze waliohusika kuwapa mimba hizo kisha wachukuliwe hatua.
Alisema, katika kikao cha bodi, mwanafunzi aliyetoroka wakati wa kupima alipatikana baada ya wazazi wake kubanwa na uongozi wa shule, ambapo alimtaja mwanafunzi mwenzake wa shule ya Sekondari ya Msakwalo (jina tunalo) kuwa ndiye aliyempa ujauzito huo. Lakini yule wa kidato cha kwanza (majina tunayahifadhi) akamtaja Padri Simpinge na kwamba ilikuwa ni wakati alipokuwa akiuza duka la Parokia.
Mwanafunzi huyo alifafanua kwamba Oktoba mwaka jana alichukuliwa kwenda kuuza duka la Parokia ya Farkwa wakati akisubiri matokeo yake ya darasa la saba.
Alisema mwezi Novemba, siku na tarehe ambayo haikumbuki, 'Baba' Paroko huyo alimtaka waende wakafanye mahesabu ya mauzo ofisini kwake na walipoingia ndani, Paroko huyo akafunga mlango na kuanza kumpapasa, baadaye akamwangusha chini na kumbaka.

No comments:

Post a Comment