.

.

.

.

Monday, November 24, 2008

ONYESHO LA JAHAZI MODERN TAARAB JIJINI LONDON JUMAMOSI TAREHE 13 DESEMBA 2008


Na Mwandishi Maalum, Uingereza.
KUNDI la muziki wa taarabu la Jahazi Modern Taarab litajumuika na Watanzania wengine London katika sherehe ya sikukuu ya Uhuru itakayofanyika katika ukumbi wa Silverspoon uliopo pembeni ya uwanja wa Wembely Decemba 13 mwaka huu.
Akizungumza jana Mkurugenzi wa Masoko ya kampuni ya Jambo Publications iliyoratibu onyesho hilo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania Uingereza ,Juma Mabakila alisema maandalizi yote ya onyesho hilo yamekamilika na iliyobaki ni siku yenyewe kuwadiatu.
Mbali na Jahazi, pia onyesho hilo litapambwa na msanii, Vicky Kamata ambae atatambulisha nyimbo zake zilizopo katika albamu yake mpya inayotarajia kuitoa hivi karibuni. Vicky ni msanii aliyejipatia sifa kubwa Tanzania, lakini hivi sasa hivi anasoma hapa London.
Mabakila alisema kundi zima la Jahazi lenye wasanii 14 linatarajia kuwasili nchini Decemba 9, tayari kwa onesho hilo, lakini hakutaka kusema kama mara baada ya onesho hilo kundi hilo litafanya onesho lingine katika mikoa mingine ya Uingereza kwa kuwa bado hawajajuwa.
“ Sasa hivi tunafanya mipango ya onesho hilo la tarehe 13, hayo maonyesho mengine bado hayapo kwenye programu yetu, lakini tutaweza kujua mara baada ya kuwasili kwa kundi hilo na kujua nini cha kufanya, lakini kwa sasa ni onesho moja tu” alisema Mabakila.
Aliwataja wanamuziki wanaokuja na kundi hilo ni pamoja na kiongozi wa kundi hilo, Mzee Yusuph, Habiba Mang’ita,Ali Nasibu, Leila Abdallah, Fatuma Masoud, Miraji Mohamed, Musa Mkenda Musa, Jumanne Ulaya,Fikirini Urembo, Rashid Nassoro na Isha Makongo.

Kundi la Jahazi hivi sasa linawika na nyimbo zake kama kazi ya Mungu haiingiliwi, nakula kwa nakshi nakshi’, Sichoki kustahamili, Shukrani ya punda,Katu hatorudi kwako, nimemshika habanduki, mtasema sana lakini hapa ndio amefika na nyingine nyingi.
Katika onyesho hilo, lililodhaminiwa na kampuni ya Guardian Limited ya Tanzania litakuwa na chakula cha usiku, litaongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maanajar Sinare.

No comments:

Post a Comment