.

.

.

.

Tuesday, November 25, 2008

YA HOSEA NA MWANYIKA YAKO NJIANI

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema kuwa hatima ya Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, itawekwa hadharani muda mfupi ujao baada ya vigogo hao kutajwa kwenye kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji wa umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond.
Mbali na hatima ya vigogo hao kuwekwa bayana muda mfupi ujao, kashfa zingine mpya zilizo ndani ya sakata la Richmond zimegundulika na zitawekwa hadharani katika muda huo, Waziri Pinda aliwaambia wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jana.
Kauli ya Pinda imekuja wiki moja baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kukana kuwa anashughulikia suala la vigogo hao waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo ya Richmond.
Akizungumza na wahariri jana ofisini kwake, Waziri Mkuu Pinda alisema yeye na timu yake wanakamilisha taratibu na kila kitu kitawekwa hadharani.
"Mimi ndiye msimamizi wa kile kikosi cha kazi kilichopewa jukumu na Bunge kushughulikia utekelezaji wa hili suala... napenda nilizungumzie wazi kuwa litafahamika ndani ya muda si mrefu," alisema Waziri Pinda.
"Nafahamu Watanzania wanayo shauku kubwa kujua nini kimejiri na kama wakuu hao walihusika au hawakuhusika, ndiyo maana kila kukicha serikali iko makini kushughulikia suala hilo na mengineyo yanayoleta utata.

No comments:

Post a Comment