.

.

.

.

Sunday, January 18, 2009

NGOME YA WACHAWI

WAZEE wa Kijiji cha Manyaji wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamedai kuwa eneo ambalo yamegundulika mafuvu 40 ya binadamu ni ngome kuu ya wachawi ambayo walikuwa wakiitumia kuwahifadhi watu wanaowachukua kimazingira wakiwa hai, maarufu kama misukule.
Walisema watu hao maarufu kama Gamboshi nguvu zao za giza zilikuwepo kwenye eneo hilo katika kipindi cha miaka ya 1950, 1960 na 1980 lakini baadaye zilianza kupungua nguvu kwa kadri wamiliki wake walivyokuwa wakipungua kwa kufariki dunia.
Katika hali hiyo, walieleza kuwa misukule hiyo iliachwa bila usimamizi bila dawa wala chakula hadi mauti yao yalipowakuta na jamii sasa kuanza kushuhudia maajabu hayo ya dunia.
"Hili tukio limetushtua sana, hatujawahi kulishuhudia tangu kuzaliwa," alisema mzee wa makamo, Joseph Tungu alipokuwa akishindwa kuelewa namna mafuvu hayo yalivyoweza kupatikana kwenye mbuyu ambao walikuwa wanauona kila siku bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea eneo hilo.
Tungu alielezea juu ya kuwepo matukio mengi ya watu kufariki dunia katika kijiji hicho tangu mwaka wa 1959 na kutaja moja ya tukio la mtoto wa kaka yake, Niga Tungu ambaye alikuwa na umri wa miaka miwili kukwapuliwa na fisi anayesadikiwa kuwa wa nguvu za giza.

1 comment:

  1. Kama kweli ilikuwako "taaluma" hiyo ya kuweza kuwachukua watu misukule, kwa nini hao waliokuwa wnaifahamu hawakuweza kuifunza kwa watu wengi zaidi (hasa watoto wao) na kuibadilisha ifanye mabo ya manufaa? Au ndio wamebadilika na kuanza kuua mazeruzeru?

    ReplyDelete