.

.

.

.

Monday, March 30, 2009

MH.CHENGE APANDISHWA KIZIMBANI

Aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Andrew Chenge leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu baada ya gari aliyokuwa akiendesha kugonga Pikipiki aina ya Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili.Mwendesha mashtaka wa Polisi David Mwafimbo alitaja makosa yanayomkabili Chenge kuwa, mawili ni ya kusababisha vifo na kosa la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe barabarani ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka yote.Kesi hiyo inaunguruma mbele ya Hakimu Emerius Mchauru na imeahirishwa hadi April 30 mwaka huu ambapo kigogo huyo anapeta nje kwa dhamana ya shilingi Milioni moja chini ya mdhamini mmoja.
Mkewe pia alitinga mahakamani kusikiliza kesi ya mumewe

No comments:

Post a Comment