.

.

.

.

Tuesday, May 26, 2009

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU HANIF ALOO AKA VICTORIA


PICHA HII NI YA MAREHEMU ALIPOKUWA AMELAZWA MUHIMBILI
Jina lake halisi ni Hanif Aloo. Huyu kijana ana asili ya kihindi (na pengine ana damu kidogo ya kichaga) na alizaliwa Moshi mjini. Alikuja Dar es Salaam mwaka 1979 na kufikia mtaa wa Mikumi Magomeni kwa Bwana mmoja mchaga aliyekuwa ameajiriwa na Car & General ambaye inasemekana alikuwa rafiki wa marehemu babake. Wakati huo Hanif alikuwa na umri wa takriban miaka 16 au 17. Mama yake alikuwa shupavu na akiendesha kampuni ya mabasi huko Moshi. Namkumbuka yule mama (sijui kama bado yuhai) akiwa amevaa over-all na spana akiingia chini ya basi pamoja na makenika wake huku yeye akiwa amechafuka na magirisi. Alikuwa mbabe ! Dada mdogo wa Hanif (Shenaz ??) alikuwa na uhusiano na Hussein Masha, mchezaji wa Taifa Stars na Simba, miaka ya 1990's mwanzoniWanaomfahamu Hanif wanajua kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu sana na bingwa wa ndondi duniani Mohamed Ali, kiasi kuwa Hanif alisafiri zaidi ya mara moja kwenda Marekani kumtembelea (alipata kutuonyesha picha alizopiga na Mohamed Ali) na hata Mohamed Ali alipokuja hapa Tanzania Hanif alikuwa karibu yake sana. Mtu mwingine aliyekuwa na urafiki wa karibu na Hanif ni mchezaji soka nyota wa wakati huo wa Uingereza mwenye asili ya kiafrika nadhani akichezea West Ham anaeitwa Justin Fashanu. Inashangaza vipi Hanif aliweza kuunga urafiki na watu mashuhuri wa kimataifa kama hao. Aidha, Hanif pia alikuwa na uhusiano wa karibu na wanasiasa wa juu wa hapa nchini.
Mwaka 1986 Hanif alikutana na msichana mmoja wa kijapani aliyekuwa akisomea medicine pale Muhimbili, wakapendana na kuoana. Baada ya mwaka hivi walipata mtoto wa kiume na baadaye wakaenda pamoja Japan. Walikaa huko kwa zaidi ya miezi sita, waliporudi Hanif alilalamika kuwa wakwe zake walikuwa hawamtaki kabisa na wakamshinikiza binti yao watengane kwa kigezo kuwa hakupaswa kuchanganya damu na mtu asiye mjapani. Kwa zaidi ya miaka miwili, Hanif alikuwa amechanganyikiwa kwa vile mkewe alitaka amnyan'ganye mtoto arudi Japan. Wakati huohuo inasemekana mke naye aliweza kuthibitisha ushoga wa Hanif baada ya kumfumania zaidi ya mara moja.Mwishoni Hanif alikubali fidia ya pesa ili amuachie mjapan mtoto na kwa hiyo wakaachana.Hanif akatumia pesa zile kununulia kiwanja maeneo ya Mbezi Beach na akajenga nyumba ndogo pale.
Kuna wakati alipata kazi kampuni ya Kearsley's Travel agency ya mtaa wa Makunganya na nadhani hata Sykes Travel agency pia.Wakati wote huo Hanif alikata mahusiano na familia yake kule Moshi na hata muonekano wake uliashiria ugumu wa maisha. Hata hivyo alitokea kujenga uhusiano wa karibu sana na malaya wa mjini na ndio walikuwa marafiki zake wa karibu. Si ajabu katika mazingira yetu shoga kugeuka kuwadi na ndivyo Hanif alivyoishia na akawa hana kazi maalumu kwa miaka mingi.Miaka miwili mitatu iliyopita Hanif alikamatwa na Polisi kwa tuhuma ya kuendesha danguro nyumbani kwake kule Mbezi. Taarifa hii iliandikwa na magazeti kadhaa lakini kesi yake haikuweza kusimama.Inasemekana kuwa Hanif mwaka jana iliamua kuiuza nyumba yake na fedha alizopata aligharamia safari yake ya kwenda Thailand kwa ajili ya kujibadili jinsia.
Pamoja na hormones alizopewa Hanif aliporudi aliota maziwa kama mwanamke na kuanza kuendesha maisha yake kama mwanamke wa kawaida, ikiwa pamoja na kuvaa mavazi ya kike. Alipunguza sana kutoka kwenda matembezini.Inasemekana Hanif hakubakwa kama magazeti mengi yalivyotangaza, bali alitaka kujiua kutokana na matatizo binafsi inawezekana ni majuto ya kitendo chake cha kubadili jinsia, mahusiano ya kimapenzi au ugumu wa maisha. Hayo yanadhibitishwa na mama mwenye nyumba yake ambaye ndie aliye piga simu polisi baada ya kumuona hali yake imebadilika. Inasemekana pia kuwa ipo barua ambayo Hanif aliacha inayoashiria uamuzi huo.Baada ya mabadiliko hayo ya jinsia, Hanif akabadili jina na kujiiita Victoria.
Na Thomas Lyatonga (MWANA BIDII)

No comments:

Post a Comment