.

.

.

.

Tuesday, July 28, 2009

UFISADI TANESCO


Nyumba 17 zakarabatiwa kwa gharama zinazotosha kujenga 20 zenye hadhi sawa !!

Nipashe Na Sharon Sauwa

Ufisadi mpya na wa kutisha ndani ya Shirika la Umeme nchini TANESCO umebainika leo baada ya Mbunge mmoja kuuanika bungeni leo asubuhi. Aliyeanika ufisadi huo mpya ni Mbunge wa Sumve (CCM), Mheshimiwa Richard Ndasa, ambaye alidai kuna ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.4 ndani ya shirika hilo la umma. Mheshimiwa Ndasa amesema shirika hilo limetumia kiasi hicho kikubwa cha pesa (Sh. Bilioni 1.4) kwa ajili ya kukarabati nyumba 17 zilizopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam, fedha ambazo kimahesabu, zinatosha kujenga nyumba kama hizo zaidi ya 20. Akazitaja nyumba hizo zenye harufu kali ya ufisadi kuwa ni ni pamoja na ile iliyopo katika kiwanja namba 13 , Mtaa wa Pore, ambayo ilikarabatiwa kwa shilingi Milioni 600 na nyumba namba 89 iliyopo katika barabara ya Guinea, ambayo imekarabatiwa kwa shilingi milioni 250. Nyumba nyingine ni yenye namba 65 palepale Oysterbay iliyokarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni 195.Nyingine ni nyumba namba 459 iliyopo katika Mtaa wa Mawenzi ambayo imekarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni 130. Akasema Mheshimiwa Ndassa kuwa matumizi hayo ni mabaya na yanalitia doa zito shirika hilo. Aidha, akasema mbaya zaidi nyumba moja iliyokarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni 600, hivi sasa iko mbioni kuuzwa kwa bei poa ya shilingi milioni 60 kwa kigogo mmoja. Mhe. Ndasa akasema cha kushangaza ni kwamba wakurugenzi wa shirika hilo, hadi sasa hawaujui ufisadi huo.

No comments:

Post a Comment