.
.
Friday, November 27, 2009
MIKANDA YA ABIRIA KILA BASI
UKAGUZI na kamatakamata ya mabasi ambayo hayajafungwa mikanda katika viti vya abiria ilianza jana kwa mabasi yaendayo mikoani.Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Bw. James Kombe amesema shughuli hiyo imeanza baada ya kazi ya ufungaji mikanda kumalizika Novemba 26, mwezi huu.Alisema serikali ilitoa agizo hilo kwa wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani na daladala kufunga mikanda hiyo katika viti kwa hiari lakini kwa sasa wakati huo umeisha na jeshi la kikosi cha usalama barabarani limesha sambazwa kuyakamata."Kwa sasa tumejipanga vizuri na tutahikisha tunakamata mabasi yote ambayo hayajafunga mikanda na kuyafikisha kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) ili yatozwe faini kwa kukaidi kufunga mikanda hiyo kwa hiari," alisema Bw. Kombe.Alisema SUMATRA itakuwa inatoza faini kwa mabasi yasiyofunga mikanda kuanzia sh.200,000 na kuendelea ambapo shughuli hiyo inatarajiwa kuwa endelevu na baada ya kumaliza mabasi yaendayo mikoani watahamia kwa daladala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment