.

.

.

.

Friday, March 25, 2011

BALOZI KALLAGHE KUTEMBELEA SLOUGH,READING NA OXFORD

Mheshimiwa Balozi Kallaghe
---
Inapenda kuwatangazia watanzania wote waliopo Reading, Slough, Oxford na vitongoji vingine vya karibu kuwa Imeandaa ziara maalum ya Mheshimiwa Balozi Kallaghe ya siku tatu itakayofanyika katika mji wa Reading kuanzia tarehe 8-10/4/2011. Sambamba ya ziara hii Mh Balozi atapata fursa ya kutembelea shughuli mbalimbali za kimaendeleo zifanyazwo na wajasilimali wa kitanzania na pia kukutana na wanajumuia wote.
Hivyo basi kutakuwa na sherehe maalum ya kumkaribisha Balozi wetu hapa Reading tarehe 9/4/11 kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 12 jioni baada ya hapo kutakuwa na tafrija pamoja na mziki kuanzia saa 1 usiku mpaka saa 6 usiku. Tafadhali wahi mapema
Ukumbi na adreess ya kwenye sherehe
Amersham Road Youth & Community CentreAmersham Road,
Caversham,
Reading,
Berks,
RG4 5BP
Tunawomba watanzania wote mjitokeze kwa wingi ili kumkaribisha Balozi wetu. Kuja kwenu ndio kufakisha kwa ziara hii muhimu, tafadhali mjulishe mwenzio.
Ratiba Rasmi ya ziara kamili itatolewa baadaye.

Asanteni kwa ushirikiano wenu,

Mwenyekiti
Tanz- UK

No comments:

Post a Comment