.

.

.

.

Tuesday, March 22, 2011

BREAKING NEWS !!!!! FIVE STAR MODERN TAARAB YAPOTEZA 13 KATIKA AJALI MBAYA YA GARI MOROGORO
Majina ya wanataarabu wa bendi ya Five Star waliokufa katika ajali mbaya ya gari Mikumi mkoani Morogoro yamefahamika akiwemo Issa Kijoti, kiongozi wa bendi hiyo Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

Kwa mujibu wa taarifa hii ya uhakika uliyothibitishwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro (RTO) zinadai kuwa waliokufa ni 13 majeruhi 8 na kuwa baadhi ya waliokufa wapo waimbaji ,wapiga vyombo ,mcheza show na mafundi mitambo japo majina ya majeruhi yatakuja hivi punde.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi majeruhi mmoja amekufa akiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akipatiwa matibabu na kufanya idadi kufikia watu 13
Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530 BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari hayo kuanguka.

Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .

Hata hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho.
Hivi sasa ndugu wa marehemu hao wapo katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro wakiendelea kutambua miili ya wanamuziki hao

.
Mtandao huu kwa niaba ya wadau wote unaendelea kuwaombea afya njema majeruhi nane katika ajali hiyo na kumwomba mwenyezi Mungu kuzilaza roho za marehemu wote mahali pema peponi Amina

No comments:

Post a Comment