.

.

.

.

Thursday, March 10, 2011

SELIKALI KUUNDA TUME KUCHUNGUZA DAWA YA MUGARIGA


WAKATI idadi ya watu ikizidi kumiminika katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo kupata kile kinachoaminika kuwa ni tiba dhidi ya magonjwa sugu, kutoka kwa mtoa huduma Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Mwasapila, waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda leo, amesema imetuma wataalamu ambao watakwenda huko Loliondo na kuangalia kama mazingira ya eneo hilo ni hatari kwa wagonjwa na kumshauri Babu Mwasapile ili aweze kusajili dawa hiyo katika mamlaka inayohusika na madawa yaani TFDA.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Wizara hiyo leo Dr. Mponda, amesema kama Babu Ambilikile Mwasapila anataka kuendelea kufanya kazi hiyo, anatakiwa kufuata taratibu kwa kusajili dawa hiyo katika Mamlaka ya Dawa na Vyakula TFDA ili iweze kuthibitishwakwa kama haina madhara yoyote. Kwa amri hiyo ya serikali inamaanisha kwamba, watu ambao wako huko Loliondo kwa minajili ya kupata matibabu, watalazimika kuondoka huko kwa kuwa hawataweza kupata matibabu.

1 comment:

  1. Tayari wameshapigwa mkwara na USA na UNICEF kuwa mchungaji ambilikile mwasapile anaharibu dili la ARVs.

    Paperworks, paperworks huwa zina tabia ya kurudisha nyuma mambo flan-flan

    ReplyDelete