KUZALIWA kwa kondoo mwenye maneno ya kiarabu katika kijiji cha Uduru Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kumefanya kijiji kupata wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali kufika kushuhudia tukio hilo na hasa waumini wa dini ya Kiislamu.
Kondoo huyo aliyezaliwa wiki tatu zilizopita aliyekuwa na neno la kiarabu ubavuni mwake upande wa kulia lenye maana ya neno ya YASINI kwa tafrisi ya Kiswahili alisababisha waumini wa madhebuhi ya Kiislamu kumimika kijijini hapo kushuhudia tukio hilo Kondoo huyo amezaliwa katika familia ya waumini wa dini ya Kikristo amewavuta waumini wengi kijiji hapo kushudia tukio hilo la ajabu na la Kiihistoria ndani ya familia na hata ndani na nje ya wilaya na mkoa.
Akizungumzia na tukio hilo kijiji hapo mmiliki wa Kondoo huyo, Grace Eliumini Massawe (55) alisema kuwa kondoo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kuwa alikuwa na neno hilo ubavuni mwake kutokana na mama wa mbuzi huyo, kumficha ndani kwa wiki zote bila kutoka nje.
Aidha alisema kuwa baada ya kuzaliwa kondoo dume mama yake alibadilisha tabia kwani awali alikuwa akila chakula na wanzake nje jambo lililokuwa kinyume baada ya kuzaliwa kwa kondoo huyo ambapo alikuwa tofauti na kondoo wengine ambapo alianza kumlea mwanae ndani bila kumtoa nje.
Pia alipogundua kuwa kondoo ana neno la kiarabu ni baada ya kondoo huyo kutolewa nje na mama yake ambapo Grace alifikiri kuwa ilikuwa ni herufi ‘W’ yenye rangi kama dhahabu iliyofifia . “Siku kadri zilizokuwa zikizidi neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi hali iliyopelekea kutafuta msaada ili kuweza kulitambua maana yake halisi kutoka kwa waumini wa dini ya kiislamu” alisema. “Mara baada ya kufika waumini mbalimbali wa madhehebu ya Kiislamu nyumbani hapo waligundua kuwa kondoo huyo dume alikuwa ameandikwa kwa kiarabu neno lenye tafrisi ya Aya ya ‘YASINI’ ”
“Pia waumini hao walinieleza neno hilo ambalo ni muhimu sana katika kitabu kitakatifu cha quran ambalo ni kama kitovu cha kitabu hicho na pia ni moja ya sura muhimu sana ndani ya kitabu hicho kitakatifu” alisisitiza mama huyo.
Katibu wa Baraza la Waislamu mkoa wa Kilimanjaro BAKWATA Sheikh Rashid Mallya, alikiri kufika kumshuhudia kondoo huyo, nakueleza kuwa maandishi yanayosomeka ubavuni mwa kondoo huyo ni sahihi kama yanavyosomeka katika kitatu kitakatifu cha quran.
Sheikh Mallya alisema aya ya maandishi hayo katika kitabu cha quran ni moja ya sura inayoeleza mambo mazito, pamoja na kueleza kuwa kitabu hicho kinazungumzia siku za mwisho za kiama, hivyo kila mtu atengeneze maisha yake. Alisema kuwa hiyo ni ishara kubwa kwa waumini wa dini ya kiislamu, kwasababu kitabu kitakatifu cha qurani kulishushwa mwezi wa ramadhani, hivyo ishara hii katika kipindi cha mfungo mtukufu wa ramadhani ni ishara kubwa.
No comments:
Post a Comment