.

.

.

.

Wednesday, October 19, 2011

DR. JULIE MAKANI APOKEA TUZO JIJINI LONDON

DR. Julie Makani Simba
Hapa akiwa na wazazi wake Bob Nyanga Makani na Vickie Kakuyu Makani
Akiwa na Mme wake Bw.Abdu Simba na Watoto Wao

Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kukuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu) Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya Anaemia kwenye ugonjwa Sickle Cell Ni matumaini yake kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya na jamii kwa ujumla. Kwa niaba ya Watanzania wote Urban Pulse tunapenda kumpongeza DR Makani kwa mafanikio hayo.

PICHA NA HABARI KWA NIABA YA URBAN PULSE CREATIVES

No comments:

Post a Comment