.

.

.

.

Thursday, October 27, 2011

KHADIJA KOPA ATUA UINGEREZA

Akiwa na wenyeji wake Heathrow airport

Malkia wa mipasho Bi. Khadija Omar Kopa ameingia jana jijini London akitokea Dar es Salaam tayari kwa ajili ya onesho lake litakalofanyika Milton Keynes siku ya Jumamosi 29th October 2011 katika ukumbi wa The Golden Lounge, Unit 35 Baton Rd, Milton Keynes, MK2 3LH.

Akizungumza na mwandishi wa blog ya TZ-ONE ya UK Bw. Ally Muhdin, Malkia wa mipasho aliwaahidi wapenzi wake kuwa atawafurahisha na kuhakikisha wataburudika na nyimbo zake mpya na zile za zamani.

Vilevile kampuni ya African Splash promotions pamoja na Infinity Entertainment wamewaomba wapenzi wote wa Khadija Kopa kujitokeza kwa wingi kwenye ukumbi wa The Golden Lounge, Milton Keynes kwa ajili ya kuweza kumuona mwanamuziki huyo - Malikia wa Mipasho.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA ALLY MUHIDDIN

No comments:

Post a Comment