.

.

.

.

Saturday, October 22, 2011

KUMBUKUMBU


FAMILIA YA ASHURA KASHEBA WA LONDON ,TUNAPENDA KUMKUMBUKA MPENDWA BABA YETU KIPENZI SUPREME MAESTRO NDALA KASHEBA NI MIAKA 7 LEO TAREHE 22 OCT 2011 ,TOKA AMEAGA DUNIA.

UCHESHI, UPENDO NA UKARIMU WAKO KATU HAUTASAULIKA ,MAWAZO NA USHAURI WAKO UTABAKI MIOYONI MWETU.

UKO KWENYE MAOMBI YETU KILA SIKU NA TUNAKUMBUKA YOTE ULIYOYAFANYA KATIKA MAISHA UMEBAKI KUWA KUMBUKUMBU KUBWA SANA KWETU JAPOKUWA SIKU ULIPOTUTOKA ILIKUWA SIKU YA MAJONZI MAKUBWA SANA KWETU.

HATUUISHI KUKUKUMBUKA NA KUKUOMBEA BABA YETU MPENDWA.

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUPA UJASIRI MKUBWA WA KUELEWA KUWA KIPENZI CHETU UMETUTOKA.

SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI,UKAE KATIKA AMANI MPAKA HAPO MWENYEZI MUNGU ATAKAPOTUKUTANISHA TENA INSHALLAH.UNAKUMBUKWA NAFAMILIA YOTE,WATOTO WAKO WOTE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI TUNAKUOMBEA MAPUMZIKO MEMA.

MWENYEZI MUNGU AIWEKE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YAKE PAMOJA NA NDUGU WOTE WALIOKWISHA TUTANGULIA MBELE ZA HAKI.

AMIN.

WAKO KIPENZI MWANAO MARIAM.

1 comment:

  1. Poleni. Nilikutana na Mzee Ndala Kasheba mjini Bujumbura mwaka 1980, kwenye mwezi wa nne. Nilikuwa Bujumbura kufundisha Chuo Kikuu cha Burundi chini ya mkataba baina ya Tanzania na Burundi. Tuliongea vizuri, katika hoteli ya Paguidas, tukikumbushana mambo ya Dar es Salaam. Ingawa nilikuwa namfahamu Tanzania, hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza na ya mwisho kuongea naye. Alikuwa mtaratibu, mwenye maongezi mazuri. Mungu amweke mahali pema Peponi. Amina.

    ReplyDelete