.

.

.

.

Monday, October 24, 2011

TAUSI WOMEN MUSICAL CLUB YAZINDULIWA RASMI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akionesha DVD&CD alizozawadiwa na Mbunge na Mlezi wa Kikundi cha Tausi women musical Club,Zakia Meghji,alichokizindua rasmi katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel,Mjinin Zanzibar, (22/10/2011).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizindua kikundi cha Taarab cha Wanawake,Tausi Taarab wanawake Zanzibar,katika ukumbi wa Salama bwawani Hotel mjini Zanzibar.(22/10/2011)
Watoto waliozaliwa katika familia za wanamuziki wa Taarab,Neema Suri,(kulia) na Nabil Mohamed wakionesha vipaji vyao katika fani ya kupiga udi katika uzinduzi wa kikundi cha Wanawake cha Taarab,kiitwacho (Tausi Women Musical Club),uzinduzi wa kikundi hicho umefanywa na Rais wa zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa salama Bwawani Hotel juzi.(22/10/2011).
Wasanii wa kikundi cha (Tausi Women Musical Club) wakicharaza ala ya Muziki wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel.(22/10/2011).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali na wasanii wa kikundi cha Taarab cha Wanawake,(Tausi Women Musical Club)baada ya kukizindua rasmi ,katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.(22/10/2011)Picha na Ramadhani Othman Ikulu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment