.

.

.

.

Sunday, December 18, 2011

RAIS JK ATEUA MABALOZI WAPYA 8

RAIS Jakaya Kikwete amewateua mabalozi wapya wanane wakiwamo walikouwa mawaziri katika Serikali yake ya Awamu ya kwanza na kuwapangia vituo vyao vya kazi.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo jana, uteuzi huo ulianza rasmi Oktoba 12, mwaka huu na wataapishwa keshokutwa.

Walioteuliwa ni Phillip Marmo kuwa balozi nchini China, awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge. Marmo alianguka katika uchaguzi wa Jimbo la Mbulu ambalo lilichukuliwa na mgombea wa Chadema, Mustafa Akunaay,.

Kwa upande wake, Dk Deodorus Kamala ambaye awali alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki amepangiwa kuwa balozi nchini Ubelgiji. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Dk Kamala aliangushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chake, CCM

Wengine ni Dk Batilda S. Burian ameteuliwa kuwa Balozi nchini Kenya ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Katika uchaguzi wa mwaka jana, Dk Batilda aliangushwa na mgombea wa Chadema , Godbles Lema katika Jimbo la Arusha Mjini. Dk Ladislaus Komba ambaye ameteuliwa kuwa balozi nchini Uganda. Kabla ya hapo Dk Komba alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wenigne ni Shamim Nyanduga, anakwenda Msumbiji na kabla ya hapo alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Grace Mujuma ameteuliwa kuwa balozi nchini Zambia na kabla ya hapo alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Pia Rais Kikwete amemteua Mohamed Hamza kuwa balozi nchini Misri ambaye kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Zanzibar katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ali A. Saleheh ambaye alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) Dubai anakwenda nchini Oman.

No comments:

Post a Comment