.

.

.

.

Monday, January 09, 2012

HARAMBEE LONDON YAFANA


Picha ya pamoja baada ya shughuli kuisha na baadhi ya wadau waliojitokeza kuchangia
---
Siku ya Jumamosi tarehe 7 January 2011 Serengeti freight wakishirikiana na Miss Jestina Blog, Bright Future TZ pamoja na Urban Pulse walifanya harambee maalum ya kuchangia watanzania walioathirika na mafuriko yaliotokea hivi karibuni mwishoni mwa mwaka jana  nyumbani Tanzania.

Mgeni rasmi alikuwa Naibu balozi Mh Chabaka Kilumanga.  Aidha Mh Balozi aliongea na kushukuru watanzania wote walioguswa na kujitolea kwa hali na mali ili kuweza kusaidia watanzania wenzao waliokumbwa na janga hili. Misaada bado inaendelea kupokelewa na kukusanywa mpaka mwisho wa mwezi huu wa january. Hivyo basi kwa wale wote walioshindwa kuweza kufika siku ya jumamosi kutoa michango bado  nafasi ipo. Kumbuka hili ni janga letu wote tafadhali fanya sehemu yako kwa jinsi Mungu anavyokubariki. 

KWA HABARI NA PICHA ZAIDI TEMBELEA  www.missjestinageorge.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment