.

.

.

.

Monday, January 09, 2012

DR. FANUEL MARO AFARIKI DUNIA

Familia ya Dkt. Fanuel Maro wa Upanga jijini Dar es Salaam inasikitika kutangaza Kifo cha Baba yao Mpendwa Dkt. Fanuel Maro (pichani) kilichotokea jumamosi jioni (tarehe 7/1/2012) katika Hospitali ya Regency iliopo Upanga, jijini Dar es Salaam.
Msiba na utaratibu wa kusafirisha mwili kwa mazishi unafanywa nyumbani kwa Marehemu Upanga Mtaa wa Longido jijini Dar es salaam.
Ibada ya Kuaga Mwili imepangwa kufanyika katika Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam siku ya jumanne (tarehe 10/1/2012) na baada ya kufanyika kwa ibada hiyo mwili ya Marehemu utasafirishwa kuelekea Old Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa Mazishi ambayo yatafanyika siku ya Jumatano (tarehe 11/1/2012).
Mungu aiweke Roho ya Marehemu Dkt. Fanuel Maro mahala pema peponiAmina.

No comments:

Post a Comment