.

.

.

.

Thursday, February 09, 2012

MGOMO WA MADAKTARI WAMALIZIKA NA VIGOGO WASIMAMISHWA KAZIUle mgomo wa madaktari na serikali hatimae umefikia mwisho asubuhi hii baada ya waziri mkuu Mizengo Pinda kukaa meza moja na madktari na kukubaliana yafuatayo.


Kwanza Pinda aliingia mkutanoni hapo Muhimbimbili saa
saa 9:54 asubuhi kwenye ukumbi wa CPL (Central Pathology Laboratory) na cha kushangaza alipigiwa makofi na madaktari kitu ambacho hakikutegemewa na wengi kutokana na hasira walizokuwa nazo madaktari hao.


Pinda ametangaza Blandina Nyoni amesimamishwa kazi mara moja kama Katibu Mkuu na Deo Mutasiwa amesimamishwa kama Mganga Mkuu wa serikali kama sehemu ya kujibu hoja za madaktari waliogoma wakati uchunguzi ukiendelea..huku interns (Madaktari wa mafunzo) wakirudi kuendelea na kazi Muhimbili.

Pia ametangaza kuwa serikali imekubali kuongeza on call allowance toka Sh10,000 mpaka elfu 25,000 kwa specialists na 20,000 kwa madaktari wa kawaida katika kipindi cha mpito na kwenye bajeti mpya masuala ya mafao ya madaktari yataangaliwa upya...pia amesema Madaktari wapewe nyumba na Green cards lakini mpaka anaondoka hajaelezea kivipi!


Pinda pia amesema Waziri wa Afya Haji Mponda na Naibu wale Dk. Lucy Nkya watawajibishwa na Mheshimiwa Rais.

No comments:

Post a Comment