.

.

.

.

Monday, March 05, 2012

JANE MPONZI HATUNAYE TENA


Familia ya Bwana Gabriel Mponzi wa Oysterbay, Jijini Dar-es-salaam.Wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa mtoto wao Jane Mponzi "Mama Melanie" pichani kilichotokea siku ya jumapili tarehe 4/3/2012 katika Hospitali ya Agha Khan Dar-es-salaam.

Ibada ya kumuaga marehemu itafanyika Jumanne tarehe 6/3/2012 nyumbani kwa marehemu Oysterbay, Dar-es-salaam kuanzia saa 6 mchana na marehemu atazikwa Ipamba-Tosamaganga, Iringa siku ya Jumatano tarehe 7/3/ 2012.

Kwa maelezo zaidi kuhusu ratiba ya mazishi, wasiliana na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Dr. Ponziano Mponzi kupitia namba 0767 600 604.

Ndugu, jamaa na marafiki waliopo mbali, wanaweza kutuma michango yao ya kufanikisha safari ya mwisho ya kwenda kumlaza mpendwa wetu Iringa kupitia:

M-PESA- 0756 -999-900
TIGO PESA- 0713 -123- 617
AIRTEL MONEY- 0784- 615-566

Bwana ametoa na Bwana ametwaa,Jina la Bwana lihimidiwe.
Amina.

No comments:

Post a Comment