.

.

.

.

Thursday, May 10, 2012

AIR TANZANIA KULETA NDEGE MPYA

KAMPUNI ya Ndege ya Tanzania (ATCL) inatarajia kuingiza nchini ndege mpya aina ya Boeing 737-500. 

Ndege hiyo inawasili nchini leo na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Taarifa ya kampuni hiyo ilisema kuwa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108, imekodiwa kutoka kampuni ya Aero Vista iliyopo Dubai, Falme za Kiarabu (UAE). 

Taarifa hiyo ilisema tayari ndege hiyo imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) nchini Misri ilikopelekwa kwa ajili ya uchunguzi huo. 

“Wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA) wamekamilisha uchunguzi wa ndege ambayo kwa sasa ipo jijini Cairo, Misri na ndege itarejea nchini kwetu kesho (leo) hii mchana. 

“Ndege hiyo imeshawekwa nembo ya Kampuni ya ATCL na baada ya kuwasili tunategemea itaanza kufanya safari mara moja,” taarifa hiyo ilisema. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 12 kwenye daraja la kwanza pamoja na abiria 96 kwenye daraja la kawaida.

No comments:

Post a Comment