.

.

.

.

Monday, May 07, 2012

ISAYA MSANGI AJA NA ALBAMU MPYA
UJUMBE: "PAMOJA TUNAWEZA CONCERT"

DHUMUNI : Kusaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kansa (Cancer) katika hospitali ya Ocean Road. Ukinunua CD/VCD, Tshirts za shetani imekula kwako utakuwa umechangia.
Kasha mbele
 Kasha nyuma
--------------------------------
Dr Isaya Msangi baada ya  kuona kilio kutoka kwa wagonjwa  wa kansa nchini Tanzania, ameona na yeye achangie mchango wake kwa kupitia uimbaji, ambapo ameamua kufanya uzinduzi wa albamu yake inayoenda kwa jina la "Shetani Imekula Kwako" ambayo ina ujumbe mkali wa kumuangamiza shetani na kazi zake zote. Dr. Isaya amesema, "Ukinunua CD/VCD na tshirts zenye ujumbe wa Shetani Imekula Kwako utakuwa umechangia katika kuokoa maisha ya Watanzania wanasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa (Cancer). akizidi kuongea amesema kutoa ni moyo na sio utajiri.

Dr. Isaya Msangi amekuja kummaliza shetani kwa kumtwanga kwa wimbo wenye ujumbe mkali ambao unamsumbua shetani kila ukipigwa maredioni na  shetani amebaki akishangaaa na kukosa nguvu za kuwavamia watoto wa Mungu. "Shetani imekula kwako" ndiyo albamu ya Dr Isaya Msangi ambayo itazinduliwa na sasa iko sokoni.

Tamasha litafanyika:        Biafra-Kinondoni jijini Dar es Salaam
Muda:                               Saa 1:30 mchana mpaka 12:30 jioni
Tarehe:                              03-06-2012
Kiingilio:                          Hakuna kiingilio
Waimbajiwatakaoshiriki:  Faraja Ntaboba, Charles Thobia, Malya, Daniel Thomas, Math Baraka, Jennifer Mgendi, Sifa John, Bony Mwaitege, Sarah Mvungi, DP,  Victor Aron, Enock Jonas, Sam Kabata, Unit Family, Overcomers Singers na wengine wengi

UNAWEZA KUCHANGIA KWA KUNUNUA TSHIRTS HIZI:


------------------------------------------
Nyimbo zinazopatikana katika Albums
1. Shetani imekula kwako
2. Shuka Bwana
3. Jehova Baba
4. Huruma ya Bwana
5. Doctor
6. Yelewi
7. Gongo la Mboto


 -------------------------------
Wasiliana nasi kwa:
Simu: +255 719 385779 | +255 689 554828
Barua Pepe: isayamsangi@yahoo.com

Uzinduzi huu umedhaminiwa na: Rumaafrica, Uncle Jimmy, Eck Production, ITC

No comments:

Post a Comment