.

.

.

.

Sunday, May 06, 2012

SIMBA WAINYUKA YANGA MABAO 5 KWA MTUNGI


Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa  kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii  kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo, Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza.  

Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga  goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari  


Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe  leo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha Medali mtoto wa mchezaji Uhuru Selemani wa Simba.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha medali mshabuliaji wa Simba Emmanuel Okwi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia na kocha wao kwa kumbeba juu juu.
Luninga kubwa ya uwanjani ikionyesha magoli yaliyofungwa na Simba

No comments:

Post a Comment