.

.

.

.

Sunday, May 06, 2012

LEO TAIFA NI SIMBA NA YANGA


Kikosi Cha simba


kikosi cha yanga

KUELEKEA pambano la leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baina ya mahasimu wa soka ya nchini, Simba na Yanga, hali ya mambo kwa Wanajangwani ilikuwa bado tete, baada ya jana kuwapo kwa mvutano mkubwa kati ya wachezaji na uongozi wa klabu hiyo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutoka Bagamaoyo jana, baadhi ya wachezaji ambao waliomba kutoandikwa majina gazetini, walisema kwamba walikuwa kwenye mpango wa kugomea mechi hiyo iwapo wasingelipwa mpaka jana jioni.

“Kaka hivi tunavyoongea nawe msimamo wetu wachezaji wote wa Yanga ni kutocheza mechi ya kesho (leo) dhidi ya Simba kwa sababu hatujalipwa posho zetu katika mechi 15 zilizopita na mishahara ya miezi miwili sasa tunajua tukicheza mechi hii ambayo ni ya mwisho hatutalipwa tena, kwa hiyo wakiweza viongozi wenyewe wakacheze,” alisema mmoja wao na kuungwa mkono na wenzake.

Walieleza kuwa baada ya kuweka msimamo huo uongozi uliahidi kwenda na pesa zao hiyo jana hivyo walikuwa wakiwasubiri kuona kama watatekeleza na walipotafutwa kwa simu kuzungumzia suala hilo, Msemaji wa Yanga, Luis Sendeu na Mwenyekiti wake, Lloyd Nchunga, hawakupatikana hewani.

Wakati yakiwa hivyo Jangwani, Wekundu wa Msimbazi, timu ya Simba, wao jana walitua jijini Dar es Salaam majira ya saa 5:30 asubuhi kwa ndege wakitokea visiwani Zanzibar walikopiga kambi.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari wa Wekundu hao Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kikosi chao kimetua salama salmini na kipo tayari kwa mechi ya leo.

Aliwaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa, ili waungane katika kushangilia ubingwa wao wa Ligi Kuu.

Aidha, wakati Yanga na Simba zikitarajia kupimana ubavu katika pambano hilo, mechi nyingine sita zitakazohusisha timu 12 za ligi zinatarajiwa kupigwa leo, katika hitimisho la ligi msimu huu wa 2011/12, ambao Simba imetwaa ubingwa, baada ya Mtibwa Sugar kuichapa Azam 2-0 juzi
.


No comments:

Post a Comment