.

.

.

.

Friday, January 25, 2013

MAMBO YA EXTRA BONGOBaadhi ya wanenguaji wa kike wa bendi hiyo, wakipozi kwa picha baada ya kushuka jukwaani.


 Mpiga Gitaa la solo wa siku nyingi aliyewahi kutamba na baadhi ya bendi kadhaa za nchini, zikiwamo Twanga Pepeta, Mchinga Sound na nyinginezo, Adolph Mbinga (katikati) akilicharaza gitaa wakatia alipopanda jukwaa la bendi ya Extra bongo kwa ajili ya kuwasalimia alipotembelea katika onyesho la bendi hiyo lililofanyika kwenye ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. 'Wasanii husalimiana kisanii'.
 Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki (kulia) akiimba sambamba na mwimbaji wa bendi hiyo, Ramadhan Masanja 'Banza Stone' wakati wa onyesho la bendi hiyo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Meeda, Sinza jijini Dar hivi karibuni. Katika onyesho hilo kulikuwa na mashindano kwa mashabiki la kucheza miondoko na staili za bendi hiyo za kizigo, ambapo washindi walikabidhiwa zawadi ya fedha taslim, sh. 100,000 kwa mshindi wa kwanza na wa pili 50,000.
 Shabiki wa bendi hiyo akimtunza Banza Stone.
 Wanenguaji wa bendi hiyo, wakishambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo.....
 Rapa wa Bendi ya Extra Bongo, Kabatano (nyuma) akiwachezesha wanenguaji wa bendi hiyo, kwa rap mpya wakati wa onyesho la bendi hiyo.


No comments:

Post a Comment