.

.

.

.

Thursday, March 07, 2013

KABURU AACHIA NGAZI MSIMBAZI

MAMBO ndani ya klabu ya Simba yamezidi kuwa hovyo baada ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu'  naye kutangaza kujiuzulu.

Kaburu anakuwa kiongozi wa pili wa klabu hiyo kwa leo kuachia ngazi ambapo aliyefungua milango alikuwa Mjumbe wa kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa kamati ya Usajili, Zacharia Hanspoppe.

Viongozi hao wamefikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo mzima wa klabu hiyo ambayo hivi karibuni imekuwa ikifanya vibaya kwenye michezo yake ya ligi kuu soka Tanzania Bara, kabla ya kutolewa kwenye ligi ya Mabingwa Afrika na Recreativo do Libolo ya Angola kwa jumla ya mabao 5-0.

Habari zilizopatikana jino hii zinaeleza kwamba Kaburu ameiwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa njia ya barua pepe kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhajj Ismail Aden Rage ambaye kwa sasa yupo nchini India akitibiwa mgongo.

Aidha, Poppe naye amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwake kwa Katibu Mkuu wa timu hiyo, Evodius Mtawala ambaye amethibitisha kupokea barua hiyo na kusema pia amepokea barua pepe ya Kaburu


.IMETAYARISHWA NA DINA ISMAIL BLOG

No comments:

Post a Comment