DAR ES SALAAM, Tanzania
Jengo la TTCL, Makao makuu, EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa 1:20.
Moto huo ulikuwa unawake katika ghorofa ya sita ya jengo hilo na ulikuwa unawake katika vyumba vitatu kwa mara moja.
Habari Mseto ilifanikiwa kufika mapema katika jengo hilo na kukuta pilika nyingi za wafanyakazi kuondoa magari yao, na magari ya shirika hilo kongwe nchini.
Magari ya kikosi cha zimamamoto kutoka kikosi cha ukoaji cha Jiji la Dar es Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini kulikuwa na ubishani kati ya wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya wafanyakazi wa Zimamoto kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita kukagua jengo lakini walifukuzwa kama mbwa,
Licha ya Kikosi hicho kuwahi hawakuwa na maji yenye pressure na ngazi za nje kufika hadi ghorofani, hali iliyopelekea watu kutumia ngazi za ndani kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.
Gari ya Ultimate Security walifika mnamo saa 12:30 na kwa ushirikiano moto uliweza kufanikiwa kuzimwa.
Jengo la TTCL lenye ghorofa 12 lililoshika moto katika ghorofa ya sita.
CHANZO: HABARI MSETO
No comments:
Post a Comment