.

.

.

.

Friday, November 08, 2013

DJ RANKIM RAMADHANI ALAZWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE


Baadhi ya ndugu na jamaa ambao walijitokeza katika safari ya mwisho ya Dj Rankim Ramadhani.
Sala ya mwisho nyumbani ikifanyika nyumbani kwa akina marehemu Rankim, Sinza kwa Remy kabla ya safari ya makaburini.
 Dj D White (mwenye kofia nyeusi), Abubakari Sadiq na Abdallah Mwaipaya (kushoto) wote wa Radio One, wakijiandaa kubeba mwili wa marehemu Rankim kwa safari ya kuelekea makaburi ya Sinza.
Ndugu na jamaa wakishusha kaburini mwili wa Dj Rankim.  
"Du mshikaji ndio ameshaondoka hivyo" ndivyo anavyoonekana akitafakari Dj Peter Moore (mwenye miwani nyeusi) ambaye alifanya kazi na Dj Rankim katika ukumbi wa Zhong Hua Garden, Kinondoni Morocco DSM.
Dj Bony Kilosa aka Bony love (kulia), Riziki Nyoni (mwenye shati jeupe) na Mully Mkinga (mwenye miwani) wakiwa na waombolezaji wengine katika makaburi ya Sinza.
Mkurugenzi wa Radio One, Deo Rweyunga akiwa na naibu mkurugenzi wa radio one Isack Gamba wakijadili jambo baada ya mazishi ya Dj Rankim Ramadhani makaburini Sinza.
 Dj Kimm wa East Africa Radio (mwenye fulana nyeusi) akiwa na waombolezaji wengine makaburini Sinza.


 Picha chini na juu ni ndugu na jamaa ambao walijitokeza kumpumzisha mpendwa wao, Dj Rankim a.k.a. Radio DJ.


Mtangazaji wa zamani aliyefanya kazi pamoja na marehemu Rankim katika kituo cha Radio One, Misanya Bingi (mwenye miwani) alikuwepo katika mazishi hayo.


Prosper Njau (kulia) na na Eliud Pemba wakiwa katika mazishi hayo.


REST IN PEACE RANKIM RAMADHANIHABARI NA PICHA kwa hisani ya Shaaban Tolle

No comments:

Post a Comment